Araghchi a,etoa ahadi hiyo wakati wa mkutano na Salah Fahs, mwakilishi wa Harakati ya Amal ya Lebanon mjini Tehran.
Katika kikao hicho, Fahs amewasilisha pongezi za spika wa bunge la Lebanon na mwenyekiti wa Harakati ya Amal, Nabih Berri, kwa Araghchi kwa kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa Iran.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amepongeza hatua za Berri za kuunga mkono mapambano na pia kujitolea mhanga wapiganaji wa Harakati yake ya Amal pamoja na wanachama wa Hizbullah katika vita dhidi ya hujuma za Israel dhidi ya Lebanon na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran pia amesisitiza kuhusu sera ya kimsingi ya Iran ya kuunga mkono vikosi vya muqawama katika mapambano yao halali dhidi ya utawala wa Kizayuni.
Araghchi na Fahs pia wamejadili matukio ya hivi karibuni ya kikanda, ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya Israel nchini Lebanon, hali ya mambo katika maeneo ya Wapalestina na vita vinavyoendelea vya Israel vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza.
342/