Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-: Kufuatia shambulizi la kigaidi la Israel dhini ya Iran, lililopelekea kuuawa makamanda kadhaa wa kijeshi wa Iran na wananchi kadhaa wa Iran, Ayatollah Jawad Amuli ametoa ujumbe wake. Andiko kamili la ujumbe huo ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Ulimwengu wa kimataifa na wananchi wa Iran walio na maarifa wanajua kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu Wazayuni:
﴿لاَ تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَی خَائِنَةٍ مِنْهُمْ﴾
"Na hutaacha kugundua khiyana kutoka kwao". (Qur'an 5:13)"
Kundi hili lililopotoka, lililojitoa kwenye adabu na kuachana na akili ya kawaida, haliheshimu hata watoto wa Gaza, wala halitambui heshima ya Umma wa Kiislamu.
Ni jukumu letu sasa kutekeleza amri ya Bwana wa Ghadir, ambaye alisema:
«رُدُّوا الْحَجَرَ مِنْ حَیْثُ جَاءَ»
"Ruddū al-hajara min haythu jā’a"
"Rudisheni jiwe lilipotoka."
Kwa kujiamini kwa Mwenyezi Mungu, kwa mshikamano na kwa mapambano ya dhati, lazima tulirudishe jiwe hilo kwa asili yake.
Ninatoa mkono wa rambirambi kwa mashahidi wetu – wanasayansi wa nyuklia, mashujaa wa Kiislamu, wanawake, na watoto – waliouawa kwa dhulma katika mashambulizi haya ya kinyama.
Jawadi Amuli
Siku ya Ghadir 1446 H
13 Juni 2025
Your Comment