14 Januari 2025 - 04:43
Mashindano ya Kisayansi kutoka ndani ya Nahj al-Balagha kwa Wanafunzi wa Shia wa Bamyan + Picha

Sambamba na Siku ya Kuzaliwa kwa Imam Jawad (a.s) na katika mkesha wa kuzaliwa kwa Amir al-Mu'minina Hazrat Ali (a.s), mashindano ya kisayansi na kiroho yalifanyika kuhusiana na "Barua ya 31 ya Nahj al-Balagha" katika seminari ya "Wilayat" huko Bamyan, Afghanistan.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Sambamba na hafza za kuzaliwa kwa Imam Jawad (a.s) na katika mkesha wa kuzaliwa kwa Amir al-Mu'minina Hazrat Ali (a.s) , Shindano la Kisayansi (Kiilmu) na Kiroho lilifanyika kwenye upande wa "Barua ya 31 ya Nahj al-Balaghah" katika Seminari (Hawzat) ya "Wilayat" katika jiji la Bamyan.

Maafisa wa Seminari (Hawzat) hii walisema kwamba lengo la kufanya mashindano haya lilikuwa ni kukuza elimu ya Ahlul-Bayt (a.s) na kuwafahamisha wanafunzi mawazo yenye nuru ya Amirul-Mu'minina (a.s) na kuimarisha moyo wa utafiti na udadisi.

Wanafunzi wa Kike na Kiume wa Shule ya "Wilayat" ya Bamyan, huku wakisoma kwa makini Barua ya 31 ya Nahj al-Balagha, ambayo ina ushauri wa kibaba wa Amirul Muminina (a.s) kwa Mtoto wake Imam Hassan (a.s), na inayojulikana zaidi kama moja ya vyanzo vya Kimaadili na Kimalezi, walishiriki katika shindano hilo la Kisayansi na kiroho.