14 Januari 2025 - 04:45
Rasimu ya kisheria nchini Uholanzi ya kuwafunga wabebaji wa Qur'an Tukufu!

Vyanzo vya Uholanzi vilifichua mswada wa kisheria uliopendekezwa na chama cha mrengo wa kulia "Geert Wilders" kwamba wale ambao wana nakala ya Qur'an Tukufu, watafungwa jela kwa miaka mitano.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Vyanzo vya Uholanzi vilitangaza kwamba chama cha siasa kali cha mrengo wa kulia cha Uhuru kinachoongozwa na Geert Wilders, ambacho ni chama kikubwa zaidi kinachounda Serikali, kinapanga kupendekeza muswada ambao mtu yeyote ambaye atakuwa ana Qur'an katika milki yake, basi atafungwa miaka mitano jela.

Ingawa chama cha Wilders hakikufichua suala hili, Mbunge "Pieter Herman Omtzigt", Kiongozi wa chama cha "New Social Contract", ambacho ni moja wa vyama vinavyoshiriki katika Muungano wa Serikali, alisema katika mahojiano ya televisheni na Rick Niemann wa gazeti la WNL op Zondag kwamba chama cha "Wilders" kinatayarisha rasimu ya Sheria ambayo imeainishwa kuwa mtu yeyote ambaye atakuwa na Qur'an, atafungwa jela miaka 5.

Pieter Omtzigt alisema kuwa suala hili liliwasilishwa kwenye Baraza wakati wa mazungumzo ya kuunda Serikali.

Pia alisisitiza kuwa Chama cha "Wilders" pia kinataka kutoa adhabu za ajabu za kifungo cha muda mrefu jela kwa raia ambao, kwa mfano wale watakaoandamana na kukaa mitaani, na alijiunga na mazungumzo (ili kujadili) juu ya msururu wa hatua za adhabu kali zilizosikika kutoka katika programu zake za (Kampeni za) uchaguzi, haswa dhidi ya Waislamu, ambazo alitaka kuziwasilisha.

Geert Wilders, Mwanasiasa Mwenye itikadi kali na mjumbe wa Bunge la Uholanzi, ambaye anajulikana kwa uadui wake dhidi ya Waislamu na hasa raia wa Morocco, alieleza kutoridhishwa kwake na ongezeko la idadi ya Waislamu nchini Uholanzi.

Kwa miaka mingi, Geert Wilders amekuwa akijaribu kueneza jumbe za chuki dhidi ya Waislamu ili kuwafukuza kutoka nchi hii.

Mnamo 2021, chama chake kiliahidi katika ilani yake ya uchaguzi ya 2021-2025 kuunda "Wizara ya Kusafisha (Kufuta) Uislamu". Pia aliahidi kuuarifisha Uislamu kuwa ni kama "Fundisho la Kiimla (Kidikteta)", na kupiga marufuku Misikiti na Shule za Kiislamu, na kuzuia kuenea kwa mawazo ya Kiislamu kupitia Qur'an Tukufu.

Mpango wa Uchaguzi wa chama chake pia ulijumuisha kupiga marufuku uvaaji wa Hijabu katika maeneo ya umma, kusitisha maombi ya hifadhi na kufunga vituo vya wakimbizi...

Geert Wilders, amekuwa akiishi chini ya ulinzi wa Polisi tangu mwaka 2004 baada ya kupokea vitisho vya kuuawa. Yeye ni mpinzani mkubwa wa Uislamu na uhamiaji nchini Uholanzi na anatumia kikamilifu akaunti yake ya Twitter kuwashambulia Waislamu na wale wanaotafuta hifadhi nchini Uholanzi.