14 Januari 2025 - 21:04
Lau si Ali (Amani iwe juu yake), Utume wa Manabii wote kuanzia kwa Nabii Adam hadi Khatamul Anbiyaa (s.a.w.w) ungekuwa haujakamilika

Hadhrat Ayatollah Wahid Khorasani alifafanua akisema: Kama si Amirul-Mu'minina Ali (amani iwe juu yake), ujumbe wote wa Manabii kuanzia Adam hadi Khatam ungekuwa haujakamilika.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la ABNA na kwa kunukuliwa na Shirika la Habari la Hawzat, Ayatollah Wahid Khorasani alizungumzia suala la Daraja ya juu ya Ali (a.s) na nafasi yake ya juu katika uumbwaji kwenye Mnasaba wa kuzaliwa kwa Hadhrat Ali (a.s) na akasema: Lau si Amirul-Muuminina Ali (amani iwe juu yake), utume wote wa Mitume (Manabii) kuanzia Adam hadi Nabii wa mwisho, ungekuwa haujakamilika... Mafunuo yote ya vitabu kuanzia Suhufi hadi Qur'an yangekuwa hayajakamilika.