Katika video iliyowekwa kwenye jukwaa la kijamii la X, shirika la Euro-Mediterranean Human Rights Monitor lenye makao yake Geneva huko Uswisi limesajili matukio ya kutisha ya ndege zisizo na rubani za Israel zinazotangaza vitisho kwa raia, na kuwaonya juu ya uwezekano wa kutokea uharibifu zaidi.
Moja ya jumbe za kutisha zilizotumwa kutoka kwa ndege zisizo na rubani za Israel kwa wakazi wa Gaza ulisema kwa kutisha: "Iwapo hautaamka kutoka kwenye usingizi, watakuletea Nakba ya pili na ya tatu", kisha sauti ya ambulensi inasikika.
Nakba au Janga, ilikuwa operesheni ya kufutwa jamii ya Wapalestina 800,000 kutoka kwenye ardhi yao, wakati Israel ilipounda dola lake haramu huko Palestina mnamo 1948. Tangu wakati huo, karibu miji na vijiji 530 vya Palestina vimefutiliwa mbali na ramani na utawala katili wa Israel.
Mbinu hii ya vita vya kisaikolojia na Israel si mpya na inaashiria mwendelezo wa mbinu zilizotumika katika kipindi cha miezi 16 ya vita vya mauaji ya kimbari ambapo zaidi ya Wapalestina 50,000 wameuawa shahidi, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
342/
