Kituo cha Uadilifu wa Kimataifa cha Australia (ACIJ) kilitangaza katika taarifa yake Jumanne iliyopita kwamba mashirika ya kiraia yanatoa wito kwa waitifaki wote wa serikali katika mnyororo wa uzalishaji wa vipuri vya ndege za kivita aina ya F-35, ikiwa ni pamoja na Australia, kusitisha haraka iwezekanavyo kuupatia utawala wa Kizayuni wa Israel vipuri na vifaa vya ndege hizo kwa njia ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja. Nchi washirika katika utengenezaji wa vipuri vya ndege za kivita za F-35 zikiwemo Australia, Canada, Denmark, Italia, Uholanzi, Norway, Uingereza na Marekani hadi sasa hazijatoa jibu kwa matakwa ya mashirika ya haki za binadamu kuhusu kuacha kuipatia Israel vipuri vya ndege hizo. Pande zilizosaini wito huo ni pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Ulaya, Marekani na Asia na pia Ulimwengu wa Kiarabu.
Nchi za Magharibi, hasa Marekani ikifuatiwa na Ujerumani na Uingereza, ndizo zinazoudhaminia pakubwa silaha utawala wa Kizayuni. Nchi hizo hasa Marekani, zilikuwa na nafasi kubwa katika kudhamini zana za kijeshi na silaha za aina mbalimbali kwa Israel katika vita vya miezi 15 dhidi ya watu wa Gaza. Marekani imeendelea kuipatia silaha Israel katika kipindi cha pili cha urais wa Donald Trump, na katika hatua ya karibuni, Trump ameagiza kutumwa Israel mabomu 1,800 ya MKA-84 ambayo utumwaji wake ulisitishwa wakati wa utawala wa Biden. Israel Katz, Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni amesisiza kuwa silaha hizo ni muhimu sana kwa jeshi la anga la utawala huo. Amesema waziri mwenzake wa Marekani ameidhinisha kuwa nchi hiyo itaendelea kuhami usalama wa Israel.
Utawala wa Kizayuni wa Israel ni miongoni mwa watumiaji wa awali wa kizazi cha tano cha ndege za kivita za F-35, na Marekani imeupatia utawala huo ndege hizo za kisasa. Jeshi la anga la Israel lilitumia ndege za kivita za F-35 kuyashambulia vikali maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza, na kuua shahidi na kujeruhi maelfu ya Wapalestina. Mashambulizi hayo pia yameharibu na kuangamiza miundombinu ya makazi na taasisi za umma katika eneo hilo.
Tel Aviv inataka kununua idadi kubwa ya ndege hizo za kivita aina ya F-35 kutoka Marekani. Ndege za kivita za kizazi cha tano za F-35 ni zinahusika katika oparesheni mbalimbali na Israel na imezitumia mara nyingi katika vita vya Gaza na mashambulizi ya anga huko Lebanon na Syria. Ili kudumisha ubora wake wa mashambulizi ya anga, uIsrael imeagiza jumla ya ndege 75 za kivita za F-35 za kizazi cha tano, ambazo zimekuwa zikifanya kazi katika jeshi la anga la utawala huo tangu mwezi Disemba 2017.
Kwa kuzingatia kuwa ndege za kivita za F-35 tangu mwanzoni zilikuwa ndege zinazozalishwa kimataifa na nchi kadhaa zinahusika katika kutengeneza wa vipuri vya ndege hizo; mashirika ya kutetea haki za binadamu yamezitaka nchi hizo ziache kuutumia utawala wa Kizayuni vipuri vya ndege hizo. Pamoja na hayo, inatazamiwa kuwa nchi hizo, hasa Marekani hazijatilia maanani ombi hilo la kimataifa na zitaendelea kuunga mkono na kuisaidia mashine ya mauaji ya Israel kwa kuipatia misaada ya kiufundi na kilojitsiki ya ndege za kivita za F-35.
Marekani ambayo ni mshirika wa kistratejia wa Israel imekuwa na nafasi kuu katika mshambulizi ya kikatili na mauaji ya kimbari ya utawala huo dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza kwa kutuma sehemu ya akiba ya vipuri vya ndege za kivita za Marekani ili kulihudumia jeshi la anga la utawala wa Kizayuni, hususuan kuzipakia ndege hizo kwa maelfu ya mabomu ya kupasua miamba. Marekani inapasa kutajwa kama mshirika wa moja kwa moja wa Israel katika jinai na mauaji ya kimbari ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza kwa kuzingatia misaada yake ya pande zote za kisiasa, kidiplomasia, kijeshi na kiusalama kwa Tel Aviv. Kadhalika, licha ya kuwa jinai za Israel, hasa mauaji ya kimbari ya watu wa Gaza, na vilevile kitendo cha Israel cha kutumia njaa kama silaha ili kuwaua wakazi wa eneo hilo, zinaonekana dhahir shahir, lakini Marekani inapinga hatua za taasisi za kimataifa kama Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kufuatilia na kusikiliza kesi ya jinai hizo.
Si hayo, tu bali kwa mara kadhaa Marekani imetumia haki yake ya kura ya turufu (veto) katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuihami na kuitetea Israel ili kuendeleza vita dhidi ya Gaza.
342/
