Akihutubia dhifa ya chakula cha usiku ya Mkutano wa Jumuiya ya Magavana wa chama chake cha Republican iliyofanyika mjini Washington, DC Trump amesema, Canada italazimika kulipa ushuru kwa magari, mbao na mafuta na gesi, wakati inaagiza 95% ya bidhaa zake kutoka Marekani, na akaongezea kwa kusema: "nadhani itawapasa wawe jimbo la 51".
Rais huyo wa Marekani amezungumzia kilichojiri kwenye mchezo wa kimataifa wa mpira wa magongo uliochezwa mjini Montreal, Canada ambapo wananchi wa nchi hiyo walizomea wakati wimbo wa taifa wa Marekani ulipopigwa kabla ya mechi, na akasema: nadhani "mwishowe" watakuwa wakiusifu wimbo wa taifa (wa Marekani)".
Trump ameeleza kuwa itabidi wafikie makubaliano na Canada kwa sababu yeye anaipenda 'O Canada', akimaanisha wimbo wa taifa wa nchi hiyo na kueleza kwamba utaendelea kupigwa wakati nchi hiyo itakapokuwa jimbo la 51 la Marekani.
Aidha, amemwita tena Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau "gavana," na kueleza kuwa anafanya "kazi nzuri."
Trump ameeleza pia kwamba wanaendelea kuiangalia Greenland na itabidi waurejeshe mikononi mwao Mfereji wa Panama.
Katika hotuba yake hiyo, rais huyo wa Marekani ambaye ametuhumiwa na baadhi ya madaktari bingwa kuwa hana utimamu wa akili ameeleza kuwa Panama ni moja ya maajabu makubwa ya ulimwengu na akaongezea kwa kusema: "tuliijenga, na kwa sababu kimsingi China imeitwaa hatutaruhusu hilo kutokea. China inalijua hilo na Panama pia.”
Trump amedai pia kwamba nchi za BRICS "zimeachana" siku chache baada ya kuzionya kwamba itazitoza ushuru wa 150% ikiwa zitajaribu kuanzisha sarafu nyingine ya kuwa mbadala wa dola ya Marekani.../
342/
