Katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) Ijumaa, Esmaeil Baghaei, Msemaji wa wizara hiyo, ameashiria mkutano wa Februari 20, 2025 kati ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Aref na mabalozi wa nchi za Kiafrika hapa Tehran.
Baghaei ameeleza kuwa, mkutano huo uliakisi "azma ya Iran ya kuimarisha uhusiano na kupanua ushirikiano na nchi za Kiafrika katika nyanja mbalimbali zenye maslahi ya pande mbili."
Katika mkutano huo, Aref alibainisha kuwa stratejia ya serikali ya Iran, chini ya Rais Masoud Pezeshkian, inafungamana na sera kuu ya taifa hili ya kuimarisha uhusiano wake na mataifa ya Afrika.
Alisisitiza lengo la kuimarisha ushirikiano katika ngazi ya nchi mbili, kimataifa, na kikanda. "Kwa kuzingatia uwezo tulionao, na kwa kuleta pamoja na kuunganisha rasilimali zetu, tunaweza kuchangia vyema katika maendeleo ya mahusiano na kuwahudumia watu wetu," Aref alisema.
Baghaei pia ameupongezi Umoja wa Afrika (AU) kwa kuhitimisha kwa mafanikio Mkutano wake wa 38, uliofanyika tarehe 15-16 Februari, 2025 huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.
Kadhalika Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ametoa salamu zake za kheri kwa Angola, Djibouti, na Algeria, ambazo zilichukua nafasi muhimu za uongozi ndani ya AU. Katika mkutano huo, viongozi wa Afrika waliwateua Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika kutoka Angola, Mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya AU raia wa Djibouti huku Naibu wake akitokea Algeria.
342/
