Leo Jumamosi shirika la habari la IRNA limenukuu makala ya televisheni ya CNN ya Marekani ambayo inasema: Wananchi wa Canada sasa hawatumii tena nyanya za California bali wameamua kutumia za Italia. Hawatumii tena pepperoni ya Ohio na badala yake wanatumia nyama zinazozalishwa Ontario na Quebec. Hawatumii tena Coca-Cola na maji ya kaboni kutoka Marekani, na badala yake wanatumia sharbati zinazozalishwa ndani ya Canada.
Mwishoni mwa mwezi Januari 2025, Trump alizidisha vitisho vyake kwa kutaka kuinyakua ardhi ya Canada na pia kuharibu uchumi wa nchi hiyo kupitia kuziwekea ushuru mkubwa bidhaa zake.
Katika sehemu yake nyingine makala hiyo ya CNN imemnukuu Graham Palmmeter, ambaye ana duka la pizza magharibi mwa Toronto, akiwaambia wateja wake kuwa ameamua kubadilisha bidhaa zinazojaza jokofu na rafu zake ili isiweko hata bidhaa moja kutoka Marekani.
Makala ya televisheni ya CNN ya Marekani imeendelea kuandika kwamba, hisia zisizo za kawaida zilizoambatana na hasira dhidi ya Marekani zimeenea ndani ya wananchi wa Canada ambao kwa kawaida ni watu wapole na wenye heshima.
Makala hiyo pia imeandika: Tangu Trump alipotishia kutoza ushuru mkubwa kwa bidhaa za Canada na kuiteka ardhi yote ya nchi hiyo na kuifanya jimbo la 51 la Marekani, chuki na hasira dhidi ya Marekani na rais wake zimeongezeka mno miongoni mwa wananchi wa Canada.
342/
Your Comment