16 Machi 2025 - 15:14
Ansarullah: Tutabaki na Gaza kwa gharama yoyote ile

Mjumbe Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah amesisitiza kuwa, Yemen haitaacha kuiunga mkono Palestina kwa gharama yoyote ile na akasema: Kila mtu anajua kuwa Yemen ni Mwaminifu katika kujibu hujuma ya adui, na Marekani inapaswa kusubiri jibu la Yemen.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (A.S) - Abna -: Katika muendelezo wa mijadala rasmi ya Yemen dhidi ya hujuma za jinai za Marekani na Uingereza dhidi ya maeneo ya raia wa Yemen, "Mohammed al-Bukhaiti" Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah alitangaza kwamba Yemen haitarudi nyuma katika uamuzi wake wa kuunga mkono Palestina na itashikilia msimamo huo kwa gharama yoyote.

Mohammed al-Bukhaiti alisema katika mahojiano na Al-Mayadeen: "Uchokozi wa Marekani dhidi ya Yemen haukubaliki na utapelekea jibu letu la pande zote."

Aliongeza: Kila mtu anajua kwamba sisi ni waaminifu katika majibu yetu na tunawaambia wale wanaotutuhumu kuwa tumejiweka katika hatari, yeyote ambaye ameshirikiana na Wamarekani na Wazayuni ni ndio amejiweka mwenyewe hatarini.

Afisa huyo wa Harakati ya Ansarullah ameashiria: Yale yaliyofanywa huko nyuma katika suala la kuupiga utawala ghasibu wa Kizayuni na mzingiro dhidi ya utawala huo unaofanywa na Yemen yatarudiwa tena. Pia, majibu ya uchokozi wa Marekani yanakuja, na Yemen haioni tofauti yoyote kati ya utawala wa Donald Trump na Joe Biden nchini Marekani.

Mohammad Al-Bukhaiti alisema: "Yemen italipa gharama, na haijalishi ni ya dharura kiasi gani, lakini haitaacha kamwe chaguo la kuunga mkono Palestina na kukabiliana na Amerika." Kinachotofautisha vita hivi na vita vilivyotangulia ni kwamba kwa ujio wa Trump, ilidhihirika kuwa vita vya sasa ni vita kati ya Haki halisi na Batili halisi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha