Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limesema hayo katika ripoti yake maalumu na kuongeza kwamba "kila siku ya shughuli za Hamas kwa ajili ya ujenzi wake mpya ni kama mwezi mzima wa kazi kwetu."
Jambo hilo limeripotiwa na maafisa usalama na ujasusi wa Israel ambao wamekiri mafanikio inayoendelea kupata Hamas katika kipindi hiki cha usitishaji vita.
Kwa mujibu wa gazeti hilo la Kizayuni wakati wiki mbili zimepita tangu Hamas wawaachilie huru mateka mara ya mwisho, na wakati Israel inakaribia kukata kabisa msaada wa kibinadamu kuingia Ukanda wa Ghaza, tunaweza kusema kwamba Israel nayo imepoteza vielelezo vyote vya nguvu zake za kutoa mashinikizo kwa Hamas.
Sehemu nyingine ya ripoti hiyo imesema kwamba, duru za usalama na ujasusi za Israel zimekaa na kutathmini mafanikio ya Hamas baada ya kusitishwa mapigano na mwishowe duru hizo zimesema kwamba, kila siku ya kusitisha mapigano ni kama mwezi mzima wa matayarisho kwa Israel ya kuanzisha tena vita.
Kinyume na matarajio, udhibiti wa Hamas kwa mambo yote ya Ukanda wa Ghaza unaongezeka siku baada ya siku ambapo Hamas inaahidi kugharamia futari na mahitaji ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa waakazi wa Ghaza. Fedha hizo inazitoa kutoka taasisi mbalimbali kama vile Benki ya Ghaza. Ni kweli Israel imefunga vivuko vya kuingia ukanda huo, lakini imeshindwa kushambulia maghala ya chakula ya Ghaza.
342/
Your Comment