Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Vyanzo vya Habari vimeripoti jinai ya magaidi wa Al-Julani dhidi ya raia wawili (wasio kuwa wa kijeshi) wa Lebanon katika maeneo ya mpaka wa Lebanon na Syria.
Kwa mujibu wa ripoti hii, raia wawili wa Lebanon walioitwa "Mohammed Nouri Medlej" na "Ahmed Noors Medlej" walichinjwa na magaidi wa Al-Julani baada ya kukamatwa wakiwa katika nyumba yao katika eneo la "Al-Fazliyeh" ndani ya Lebanon.
Miili ya Mashahidi hao wawili ilipatikana baada ya kuchinjwa katika eneo la "Al-Sad Mataraba", katika makutano ya Lebanon na Syria.
Hapo awali, usiku wa jana na leo, magaidi wa al-Julani waliulenga mara kwa mara mji wa mpakani wa "Al-Qasr" katika ardhi ya Lebanon kwa maroketi, ambayo yaliacha idadi kadhaa ya Mashahidi na kujeruhiwa kadhaa miongoni mwa raia wa Lebanon.
Mpaka wa Syria na Lebanon
Your Comment