17 Machi 2025 - 18:12
Source: Parstoday
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu: Bila shaka yoyote taifa la Yemen litaibuka mshindi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amelipongeza taifa la Yemen kwa Muqawama wake wa kukabiliana na jinai za kinyama za utawala wa Marekani dhidi ya nchi hiyo na kusisitiza kuwa hakuna shaka yoyote taifa la Yemen litaibuka mshindi.

Ayatullah Khamenei ameeleza hayo katika ujumbe alioweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X na kuongeza kuwa, njia pekee ya kufuata ni njia ya mapambano na Muqawama.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kwa kusema: "jambo ambalo limeifanya Marekani na washirika wake kuingiwa na hofu leo ​​hii ni ukweli kwamba mataifa ya Kiislamu yamesimama imara na kwa uthabiti; na Muqawama huu utathibitisha kuwa athirifu na wenye ufanisi".

Wakati huohuo, Baraza la Uratibu wa Tablighi za Kiislamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetoa taarifa likilaani mashambulizi ya kivamizi na kichokozi ya Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen.

Baraza hilo limeeleza katika taarifa: kuanza tena mashambulizi ya anga ya Marekani na Uingereza dhidi ya nchi hiyo na watu wa Yemen katikati ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa mara nyingine tena kumedhihirisha hofu uliyonayo mfumo wa kibeberu kwa Muqawama shupavu wa wananchi wa Yemen na kufichua pia sura halisi ya uistikbari.

Taarifa hiyo ya Baraza la Uratibu wa Tablighi za Kiislamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeongezea kwa kusema: hatua hii ya kichokozi na kivamizi sio tu ni mfano wa wazi wa ukiukaji wa umoja wa ardhi na mamlaka ya kujitawala na ya kitaifa ya nchi huru, lakini pia ni ishara ya wazi ya kuendelea mkakati wa uingiliaji ambalo lengo lake ni kuvuruga uthabiti na utulivu katika Asia Magharibi, kushadidisha mantiki ya kuzusha hali ya mchafukoge na kuhalalisha uvamizi, ughasibu na ubeberu katika mfumo mpya wa usalama wa kikanda.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha