17 Machi 2025 - 18:16
Source: Parstoday
Israel imeficha gharama za vita

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa gharama za vita za utawala huo zimefichwa mwaka huu, tofauti na ripoti za mwaka jana, na kuna wasiwasi kuhusu usimamizi wa bajeti.

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Wizara ya Fedha ya utawala wa Kizayuni ameacha kuchapisha ripoti za mara kwa mara kuhusu gharama za vita zilizotumiwa na Israel katika vita dhidi ya Gaza na Lebanon.

Gazeti la Haaretz limeandika kuwa: Hatua hii imebua wasiwasi kuhusu kuwepo uwazi katika kusimamia bajeti ya utawala wa Kizayuni.  

Hadi mwishoni mwa mwaka jana, Mkaguzi Mkuu wa Wizara ya Fedha ya utawala wa Kizayuni alikuwa akichapisha mara kwa mara ripoti za kila mwezi za gharama za vita katika mfumo wa bajeti ya utawala huo. Hata hivyo, tangu Januari mwaka huu, uchapishaji wa ripoti hizi umesitishwa, na imekuwa vigumu kuchambua utendaji wa bajeti ya utawala wa Kizayuni na matumizi halisi ya utawala huo.

Kabla ya ripoti hizo kusitishwa, matumizi ya kijeshi ya Israeli yalikadiriwa kuwa karibu shekeli bilioni 125 yaani (kila dola ni sawa na shekeli 3.6); ambapo karibu shekeli bilioni 100 zilitumika mnamo 2024.

Haaretz imeongeza kuwa, ripoti za huko nyuma kuhusu gharama za vita zilitofautisha kati ya matumizi ya ulinzi na ya kiraia ambayo yalitoa mwanya wa kufanyika uchambuzi bora kuhusu ongezeko la matumizi la utawala wa Israel; lakini sasa kusita kuchapishwa gharama za vita za utawala huo kunaaminisha kwamba haiwezekani kukokotoa gharama halisi ya Israel baada ya kutoa gharama zake za vita. 

"Wasiwasi kuhusu gharama umeongezeka maradufu hivi sasa kwa kuzingatia matamshi ya karibuni ya Israel kuhusu uwezekano wa kuanza tena vita.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha