2 Aprili 2025 - 17:15
Mashahidi 6 na majeruhi kadhaa katika shambulio la jana usiku la Marekani dhidi ya Yemen + Video

Jana usiku, ndege za kivita za Marekani zililenga maeneo kadhaa ya Yemen, na kusababisha idadi ya mashahidi na watu kadhaa kujeruhiwa.

Kulingana na Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - Jana usiku, ndege za kivita za Marekani zilishambulia Mji Hodeidah na eneo la Saada nchini Yemen.

Kwa mujibu wa ripoti ya Al-Masira, katika jinai za hivi punde, ndege za kivita za Marekani zilishambulia kwa mabomu jimbo la "Hajjah" Kaskazini Mashariki mwa Yemen mara 3.

Watu 4 waliuawa Shahidi na watu kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la Marekani dhidi ya kampuni ya maji ya mji wa "Al-Mansouriyah" Mkoani Hodeidah.

Mtandao wa Al-Masira wa Yemen umechapisha picha za jinai zilizofanywa na Wamarekani katika shambulio la kampuni ya maji ya "Al-Mansouriyah" eneo la Hodeidah, nchini Yemen. Tizama jinai hii ya Marekani katika video hiyo hapo juu namna wanavyoshambulia Wananchi wa Yamen wasiokuwa na hatia na ambao hawana hata silaha yoyote.

Your Comment

You are replying to: .
captcha