4 Aprili 2025 - 16:34
Zaidi ya Mashahidi 30 katika jinai mpya ya Israeli katika shambulio la Shule Mashariki mwa Gaza + Video

Idadi ya wahanga wa shule hiyo iliyoshambuliwa kwa bomu katika Kitongoji cha al-Tuffah Mashariki mwa Gaza hadi sasa imefikia zaidi ya Mashahidi 30 na idadi ya waliojeruhiwa imefikia 100.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Katika jinai zaidi ya hivi punde ya utawala ghasibu wa Kizayuni na kutokana na shambulio la bomu katika shule moja Mashariki mwa Gaza, zaidi ya watu 30 wameuawa Shahidi na wengi kujeruhiwa.

Zaidi ya Mashahidi 30 katika jinai mpya ya Israeli katika shambulio la Shule Mashariki mwa Gaza + Video

Kwa mujibu wa habari, Shule ya Dar al-Arqam iliyoko katika Kitongoji cha al-Taffah Mashariki mwa Gaza ilikuwa makazi ya watu wengi wa Palestina waliokimbia makazi yao, wakiwemo Wanawake na Watoto wengi wa Kipalestina.

Idadi ya wahanga wa shule hiyo iliyoshambuliwa kwa bomu katika kitongoji cha al-Tuffah mashariki mwa Gaza hadi sasa imefikia zaidi ya mashahidi 30 na idadi ya waliojeruhiwa imefikia 100.

Duru za kimatibabu zimetangaza kuwa, idadi ya Mashahidi wa Mashambulizi ya jana (Alhamisi) ya jeshi haram na vamizi la Kizayuni katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza imefikia watu 112.

Your Comment

You are replying to: .
captcha