5 Aprili 2025 - 15:43
Video + Mwanachuoni huyu wa Kisunni anasema "Sisi tunajikurubisha kwa Allah kwa kumpenda Hassan, na Hussein, na Fatima na Ali"

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Mwanachuoni huyu wa Kisunni anasema "Sisi tunajikurubisha kwa Allah kwa kumpenda Hassan, na Hussein, na Fatima na Ali. Ama Ali bin Abi Talib (a.s) kumzungumzia kunahitajia ratiba kamili. Lakini inanitosha kumzungumzia Ali (a.s) kwa maneno aliyoyasema Mtume (s.a.w.w) kumhusu kwamba: " Je, huridhii wewe kuwa na daraja kwangu mimi kama ile aliyokuwa nayo Harun kwa Mussa (a.s), ispokuwa hakuna Nabii baada yangu?!. Kisha akasema Mtume (s.a.w.w) kuhusu Ali (a.s) siku ya vita vya Khaibar: "Hakika kesho nitampa Bendera hii mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda.Mwenyezi Mungu ataileta ushindi wa Khaibar kupitia (mtu huyu).Yeye kamwe hakimbii vitani."".

Ama Ali bin Abi Talib (a.s) kumzungumzia kunahitajia ratiba kamili

Video + Mwanachuoni huyu wa Kisunni anasema "Sisi tunajikurubisha kwa Allah kwa kumpenda Hassan, na Hussein, na Fatima na Ali"

Lakini inanitosha kumzungumzia Ali (a.s) kwa maneno aliyoyasema Mtume (s.a.w.w) kumhusu kwamba:

 "أَمَا تَرْضَی أَنْ تَکونَ مِنِّی بِمَنْزِلَةِ هَارُونَ، مِنْ مُوسَی إلا أنه لا نبي بعدي" (راجع: بخاری، صحیح البخاری، ۱۴۰۱ق، ج۴، ص۲۰۸، ج۵، ص۱۲۹، مسلم نیشابوری، صحیح مسلم، دار احیاءالتراث العربی، ج۴، ص۱۸۷۰ و ۱۸۷۱.).

"Je, huridhii wewe kuwa na daraja kwangu mimi kama ile aliyokuwa nayo Harun kwa Mussa (a.s), ispokuwa hakuna Nabii baada yangu?!".(Rejea: Bukhari, Sahih Bukhari, 1401 AH, Juzuu ya 4, Ukurasa wa 208, Juzuu ya 5, Ukurasa wa 129. Muslim Neishabouri, Sahih Muslim, Dar Ahya al-Trath al-Arabi, Juz. 4, ukurasa wa 1870 na 1871​​).

Kisha akasema Mtume (s.a.w.w) kuhusu Ali (a.s) siku ya vita vya Khaibar:

"لأُعْطِیَنَّ الرَّایَةَ رَجُلاً یُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَیُحِبُّهُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ یفتح الله علی یدیه لیس بفرار" . (راجع: ابن هشام، السیرة النبویة: ج۳، ص۷۹۷، القاهرة: مكتبة محمد علی صبیح وأولاده).

"Hakika kesho nitampa Bendera hii mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda.Mwenyezi Mungu ataileta ushindi wa Khaibar kupitia (mtu huyu).Yeye kamwe hakimbii vitani."(Rejea: Ibn Hisham, Al-Sirah al-Nabawiyyah (Sirah ya Mtume): Juzuu ya 3, Ukurasa wa 797, Cairo: Maktaba ya Muhammad Ali Subih na Wanae).

Your Comment

You are replying to: .
captcha