19 Agosti 2025 - 22:19
Matembezi ya Kumbukizi ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) Kuandaliwa Dar es Salaam kupitia Hawzat Imam Swadiq (as)

Tukio hili linatarajiwa kuwa jukwaa la mshikamano wa Kiislamu na nafasi ya kumuenzi Mtume wa Rehema (s.a.w.w) kwa ibada, dua na kuonesha mapenzi yetu kwake.

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Hawzat Imam Swadiq (as) imetangaza rasmi kuwa imeandaa Matembezi ya kumbukizi ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), Mbora wa Walimwengu na Kiongozi wa Waumini, yatakayofanyika Siku ya Ijumaa tarehe 22 Agosti 2025.

Matembezi hayo makubwa yatakutanisha Waumini wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na vitongoji vyake, ambapo msafara utaanzia Ilala Boma hadi Viwanja vya Pipo, Kigogo Post, Jijini Dar-es-Salaam

Tukio hili linatarajiwa kuwa jukwaa la mshikamano wa Kiislamu na nafasi ya kumuenzi Mtume wa Rehema, Muhammad (s.a.w.w) kwa ibada, dua na kuonesha mapenzi yetu makubwa kwake (s.a.w.w).

Viongozi wa Dini na Wanazuoni mbalimbali wanatarajiwa kushiriki na kutoa hotuba zitakazogusia maisha ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), mafundisho yake ya kiroho na mchango wake wa kudumu kwa ustaarabu wa Mwanadamu.

Kwa mujibu wa waandaaji, matembezi haya ni mwendelezo wa juhudi za kuimarisha mshikamano wa waumini na kufikisha ujumbe wa upendo, amani na uadilifu ambao Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliuishi na kuufundisha.

Hawzat Imam Swadiq (a.s) imewaalika waumini wote na wananchi kwa ujumla kushiriki katika tukio hili adhimu na lenye kumbukumbu ya kihistoria. Kama ilivyoashiriwa hapo juu, Matembezi haya yatafanyika Siku ya: 

Ijumaa, Tarehe: 22/08/2025. Sehemu ya kuanzia: Ilala Boma hadi Viwanja vya Pipo, Kigogo Post - Dar-es-salaam.

Nyote mnakaribishwa kwa heshima kubwa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha