Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlal-Bayt (a.s) - ABNA - Katika makala hii fupi, tutaeleza ni jinsi gani tunavyoweza kutoharisha vitu vilivyo najisika kwa kutumia maji. Na tunasema kwa kutumia maji kwa kuwa maji ndio yaliyochukua nafasi kubwa katika kutoharisha vilivyonajisika kuliko vingine vyote vyenye kutoharisha.Tutamia herufi (S) kuashiria swali na herufi (J) kuashiria jibu lake.
S_1- Maji halisi (Mut-laq) yanatoharisha kitu gani?
J_1- Maji halisi yanatoharisha kila kitu kilicho najisika, hata maji yenyewe yakiwa yamenajisika hutoharishwa kwa maji halisi. Maji machache yakinajisika yatatoharika kisheria kwa kuunganika (au kuunganishwa) na maji mengi, lakini pia maji hayo ambayo ni maji mengi yasiwe yamebadilika kwa kupitia najisi.
S_2- Kuna sharti gani wakati wa kutoharisha kitu kilicho najisika?
J_2- Kume shartishwa kabla ya kutoharisha kitu kilicho najisika kufanya haya yafuatayo: Kabla ya yote ni kuondoa najisi ile, pamoja na kusugua na kukamua.
S_3- Ni ipi hukumu ya maji yaliyo tumika katika kuondoshea najisi?
J_3- Maji yaliyo tumika katika kuondoshea najisi hukumu yake ni najisi, yaani (yamenajisika) na wala hayafai kuondoshea najisi nyingine.
S_4- Kitu gani kinatoharika kwa maji ya mvua? na vipi kinatoharika kwa maji hayo ya mvua?
J_4- Maji ya mvua yanatoharisha kila kitu kilicho najisika, na miongoni mwavyo ni maji, ardhi, godoro, na vyombo.
Hivyo vilivyotajwa hutoharika kwa maji ya mvua kwa kuenea maji ya mvua juu yake bila ya kuhitajia kurudia rudia kuosha, na wala haihitajii kusugua wala kukamua, lakini ni wajibu (ni lazima) kwanza ile najisi iwe imeondoka (imeondoshwa).
S_5- Maji yenye kutembea au maji mengi (Kur-ru) yanatoharisha vipi kitu kilichonajisika?
J_5- Maji yenye kutembea au maji mengi yanatoharisha kitu kilichonajisika kwa kuenea kwa maji yale juu ya kile kitu kilichonajisika, pamoja na kuhitajia kusugua lakini katika kitu kinachohitajia kusuguliwa (kwa kitambaa au kwa blashi au kwa kutumia kitu chochote kile cha kusugulia.Na kitu hicho kinachohitajia kusuguliwa ni) kama vile godoro,na vitu vingine mfano wake,bila ya kuhitajia idadi (yaani hakuna idadi maalum ya kusugua bali unasugua mpaka pale ujiridhishe na kukinaika kuwa sasa najisi imeondoka,ispokuwa kama chombo kitakuwa kimenajisika kwa kunywea Mbwa au Nguruwe au amefia panya buku ndani yake (hapo katika kusugua chombo hicho kumetajwa idadi maalum ya kusugua).
S_6- Je, chombo akinywea Mbwa au Nguruwe au kufia panya ndani yake kuna hitajia idadi maalumu wakati wa kutoharisha kwa kutumia maji yanayo tembea au yaliyotuama?
J_6- Naam, inahitajia idadi kama vile unavyo toharisha kwa maji machache.
S_7- Vipi kinatoharika kitu kisichokuwa chombo kwa kutumia maji machache?
J7-Kina toharika kwa kuosha mara mbili (lakini) baada ya osho la kuondoa najisi,ikiwa kimenajisika kwa mkojo.Na kama kitakuwa kimenajisika kwa kitu kingine kisichokuwa mkojo basi inatosha kuosha mara moja .
S_8- Vipi kinatoharika chombo kilichonajisika kwa kunywea mbwa kwa kutumia maji machache ?
J_8- Kukitoharisha kwake inahitajia kukisugua kwa mchanga kwanza kisha kukiosha kwa maji mara mbili.
S_9- Vipi kinatoharika chombo kilichonajisika kwa kunywea nguruwe au amefia panya ndani yake kwa kutumia maji machache?
J_9- Kinatoharika kwa kuosha mara (7) saba,ama kikinajisika kwa kitu kingine ni wajibu kukiosha mara tatu.
Your Comment