Taarifa ya Hamas imepongeza sana msimamo wa kishujaa wa mhandisi Ibtihal Aboussad, ambaye kwa ujasiri na kwa kujitolea, alifichua ushirikiano wa makampuni makubwa ya teknolojia ya kimataifa na mashine ya mauaji ya utawala wa Kizayuni kwa namna ya kipekee."
Ripoti mbalimbali zimeeleza kuwa makampuni ya teknolojia, ikiwemo Microsoft, yamevipatia vikosi vya jeshi la Israel zana za kijasusi zilizotumika katika mauaji ya Wapalestina yanayoendelea huko Gaza, ambapo zaidi ya Wapalestina 50,000 wameuawa.
Hamas iimetoa wito kwa wafanyakazi na maafisa wote wa kampuni zenye uhusiano na jeshi la Israel kufuata mkondo huo na kuchukua msimamo sawa na wa Aboussad na wenzake
Hamas pia imeutaka Umoja wa Mataifa, jamii ya kimataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu kusajili aina zote za ushirikiano wa kiteknolojia na utawala ghasibu wa Israel, kuyafungulia mashtaka makampuni hayo kwenye mahakama za kimataifa na kuyawekea vikwazo kwa kukiuka sheria na maadili ya binadamu."
Taarifa ya Hamas imetolewa baada ya wafanyakazi wa shirika la Microsoft la Marekani kuandamana wakati wa tukio la sherehe ya miaka 50 ya kuanzisha kampuni hiyo, wakitangaza upinzani wao dhidi ya kutumiwa teknolojia ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence-AI-) ya kampuni hiyo na utawala wa Israel katika vita vyake vya mauaji ya kimbari huko Gaza.
Mmoja wa waandamanaji aliyetambuliwa kama Ibtihal Aboussad ambaye ni mfanyakazi wa Microsoft alisikika akipiga mayowe na kusema: “Mustafa, aibu kwako,” huku akielekea jukwaani. Tukio hilo lilimfanya Suleyman aache hotuba yake.
Aliendelea kusema, “Wewe ni mfanyabiashara anayefaidika na vita. Acha kutumia Akili Mnemba kufanya mauaji.”
Baadaye, mfanyakazi mwingine wa Microsoft, Vaniya Agrawal, alikatisha sherehe hiyo huko Redmond, Washington, wakati Gates, Ballmer, na Mkurugenzi Mtendaji wa sasa Satya Nadella walipokuwa jukwaani.
Wafanyakazi wengine pia walikusanyika na kuandamana nje ya ukumbi wa mkutano.
Microsoft imekabiliwa na ukosoaji unaoongezeka kuhusiana na mikataba yake na jeshi la Israel, kwani ripoti zinaonyesha kuwa teknolojia ya Akili Mnemba za kampuni hiyo hutumika kuchagua maeneo yanayolengwa kwa mabomu katika Ukanda Gaza, na kusababisha mauaji ya maelfu Wapalestina hasa wanawake na Watoto..
342/
Your Comment