12 Aprili 2025 - 23:59
Ugumu uliopo katika kuwatangaza Kizazi Kitukufu cha Mtume Muhammad (saww) ambao ni Mawalii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) | Watu hawawajui Ahlu-Bayt (as)!

Leo hii, jambo la kuwatangaza Ahlul-Bayt (a.s) ambao ndio tumeusiwa na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) tushikamane nao baada yake na kuwafuata wakiwa wakiwa kama Kizito cha Pili baada ya Qur'an Tukufu, ni jambo gumu kulingana na jamii ya watu tunayokabiliana nayo.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlu-Bayt (a.s) - ABNA - Sheikh Muhammad Abdu, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Shia Ithna Ashari Tanzania (T.I.C), amebainisha sababu za ugumu uliopo katika kuwatangaza Kizazi Kitukufu cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambao ni Mawalii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Amesema: Suala la kuwatangaza Ahlul-Bayt (a.s) sio jambo jepesi, linahitajia kumuomba Mwenyezi Mungu kulifanya kuwa jepesi. Ni kama vile Nabii Mussa (a.s) alivyomuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amfungulie kifua chake, na kulifanya jambo lake (la kuitangaza Tawhid) kuwa jambo jepesi, kwani jambo hilo ni zito mno na gumu kulingana na watu wanaoenda kukabiliana nao na kuwatangazia kuwa wanapaswa kumuabudu Mwenyezi Mungu na apaswaye kuabudiwa kwa Haki.

Ugumu uliopo katika kuwatangaza Kizazi Kitukufu cha Mtume Muhammad (saww) ambao ni Mawalii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) | Watu hawawajui Ahlu-Bayt (as)!

Leo hii, jambo la kuwatangaza Ahlul-Bayt (a.s) ambao ndio tumeusiwa na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) tushikamane nao baada yake na kuwafuata wakiwa wakiwa kama Kizito cha Pili baada ya Qur'an Tukufu, ni jambo gumu kulingana na jamii ya watu tunayokabiliana nayo. Unaweza kwenda sehemu kuwatajia watu kuhusu Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w), kwa mfano ukauliza kuhusu Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) anayeitwa:

Imam Zainul-A'bidina (a.w), mtu anashangaa na kuuliza ndio nani Zainul-A'bidina?, yaani haelewi na hamjui na hajawahi hata kusikia akitajwa kokote!, yaani mtu hajui hata kama duniani kuliwahi kuzaliwa mtu anayeitwa Zainul-A'bidina na ni khalifa katika Makhalifa kumi na wawili wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), na ni Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), na ni Walii katika Mawalii wa Mwenyezi Mungu (swt)!.

Mtu hajui kabisa kama kulikuwa na mtu ambaye ni Alim mkubwa, Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), Kiongozi na Khalifa aliyeitwa Jaafar Sadiq (a.s)!. Na sio kwamba mtu hataki kuwajua, hapana!, Bali hawaambiwi lolote kuhusu watu watukufu wa kizazi cha Mtume (s.a.w.w).

Tena wengine unakuta wanaitwa  Masheikh kabisa katika jamii zao, wasomi wa dini, ni watu wazito katika jamii, lakini hawawajui watu watukufu wa Kizazi Kitkufu cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwa sababu wameishi katika mfumo usiowawezesha kuwajua Maimam na Makhalifa watukufu wa Kizazi cha Mtume Muhammad (s.a.w.w)!, utao wao umefichwa na unafichwa kwa watu, hivyo unakuta watu hawawajui kwa sababu wamesababishwa makusudi wasiwajue, yaani wao kama wao  sio kwamba hawataki kuwajua watukufu wa Kizazi cha Mtume (s.a.w.w), bali mfumo umewaficha na kuwanyima haki ya kuwajua.

Watukufu wa Ahlul-Bayt (a.s) ni Nuru ya uongofu, lakini watu hudhamiria kuificha nuru kwa watu ili watu wasifuate nuru na kuangaziwa na mwangaza wake. Na ndio maana Mwenyezi Mungu akasema ndani ya Qur'an Tukufu:

يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ

"Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia". (Surah As-Saf, Aya ya 8).

Kwa hiyo, kazi ya kuwatangaza Ahlul-Bayt wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), sio kazi nyepesi, ni kazi nzito mno, yenye vikwazo mbalimbali kutoka kwa watu wenye nia na lengo la kuizima Nuru ya watukufu wa kizazi Kikutufu cha Mtume Mtukufu, Muhammad (s.a.w.w). Hii ni kwa sababu jamii za watu zimefanywa kutojua lolote kuhusu Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w), hivyo wakati unawafikishia lolote kuhusu Ahlul-Bayt (a.s), kwao linakuwa jambo jipya, jambo geni katika akili zao, hawana habari kabisa na Ahlul-Bayt (a.s), watu hawajui Mtume (s.a.w.w) ameusia nini Umma wake kuhusu kuwafuata Ahlul-Bayt (a.s), watu wanafuata njia zao watakazo wao, walizoamua kujielekeza wao na akili zao na wakaacha kufuata maelekezo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwa makusudi au kwa kufichwa yaliyokuwa ya haki kuhusiana na Ahlul-Bayt (a.s).

Mtu toka anaingia duniani, anamsikia ni Abu Hurayra tu kuwa ndio ndio Mpokezi wa Hadithi za Mtume Muhammad (s.a.w.w)!. Mwingine anawaza kabisa kuwa labda huyu Abu Hurayra alilelewa ndani kabisa ya Nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)!. Ni maajabu makubwa!. Maana Abu Hauryra ametajwa na maelfu ya hadithi ambazo inadaiwa amezipokea toka kwa Mtume (s.a.w.w), kiasi kwamba hakuna yeyote katika watu wa nyumba Tukufu ya Mtume (s.a.w.w), waliokuwa wanaishi nyumba moja na Mtume (s.a.w.w) asubuhi Mchana na Usiku, wanaomfikia Abu Hurayra kwa kupokea Hadithi hali ya kuwa Abu Hurayra hakuwa na miaka mingi ya kusilimu na kuwa karibu na Mtume (s.a.w.w), lakini ni ajabu Abu Hurayra anamaelfu ya Haidithi zinazosemwa kapokea toka kwa Mtume (s.a.w.w) kuliko hata Imam Ali (a.s) aliyelelewa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) akiwa mtoto mpaka anakuwa mtu mzima bali mpaka mwisho wa Maisha ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)!, na aliyeishi nyumba moja na Mtume (s.a.w.w)!.

 Lakini ajenga ni ileile ya kuficha Nuru ya watukufu wa Ahlu-Bayt wa Mtume (amani iwe juu yao), kama alivyosema Mwenyezi Mungu: 

يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ

"Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia". (Surah As-Saf, Aya ya 8).

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha