Akijibu taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ambayo pia ilionyesha matumaini ya kurefushwa usitishaji vita kati ya Russia na Ukraine baada ya Pasaka, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova amesema: "Upande wa Ukraine umekiuka usitishaji vita wa Pasaka kwa kutumia mifumo ya roketi ya Marekani ya HIMARS."
Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Russia amesema kwamba, serikali ya Kiev haikuzingatia usitishaji wa mapigano wakati wa Pasaka, na zaidi ni kwamba, silaha za Marekani zimetumiwa huko Bankova kukiuka usitishaji wa mapigano.
Zakharova amesema: "Hilo halikutokea kwa sadfa bali ni mwenendo wa serikali ya Kiev."
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameongeza kuwa wakati wa kusitishwa mashambulizi dhidi ya rasilimali na miundombinu ya mafuta na nishati, ambako Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky pia alikuidhinisha, Kiev ililenga mara kwa mara miundombinu ya nishati ya kiraia ya Russia.
Rais Vladimir Putin alikuwa amesema kuwa: "Katika hafla ya Pasaka, Russia itasitisha mapigano yote na inatarajia Ukraine kufanya vivyo hivyo na kusitisha uhasama katika kipindi hicho."
342/
Your Comment