23 Aprili 2025 - 23:36
Source: Parstoday
Viongozi wa dunia wajiandaa kushiriki mazishi ya Papa, Roma

Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Italia Roma, kabla ya mazishi ya Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia yaliyopangwa kufafanyika siku ya Jumamosi.

Italia imetangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, huku bendera zikipeperushwa nusu mlingoti kwenye majengo yote ya umma. Viongozi mbalimbali wa dunia wametangaza kushiriki maziko ya kiongozi huyo wa kiroho siku ya Jumamosi.

Hali ya usalama imeimarishwa katika mji mkuu wa Italia, Roma kabla ya ibada ya mazishi na maziko ya Papa Francis aliyefariki Jumatatu, yatakayofanyika siku ya Jumamosi. Viongozi wa ngazi za juu kutoka nchi mbalimbali za ulimwengu wanatarajiwa kushiriki.

Jorge Mario Bergoglio, ambaye baadaye alichukua jina la Papa Francis, alichaguliwa kuwa papa mnamo Machi 13, 2013, jambo lililowashangaza wengi waliokuwa wakifuatilia siasa za Kanisa, kwani padri huyo kutoka Argentina alionekana kuwa mtu wa nje ya mfumo wa kawaida.

Papa Francis alirithi Kanisa lililokuwa katika mgogoro mkubwa kutokana na kashfa ya unyanyasaji wa kingono wa watoto, pamoja na migogoro ya ndani ya utawala wa Vatikan, na alichaguliwa akiwa na dhamira ya kurejesha nidhamu na utulivu.

Hata hivyo, kadri kipindi chake cha uongozi kilivyokuwa kikiendelea, alikumbwa na upinzani mkali kutoka kwa wahafidhina waliomtuhumu kwa kuvunja mila za jadi za Kanisa. Vilevile, alikosolewa na wanamabadiliko waliodhani hakuenda mbali vya kutosha katika kulibadilisha Kanisa hilo lenye historia ndefu.

Papa Francis aliteua karibu asilimia 80 ya makadinali wapiga kura watakaomchagua Papa ajaye, jambo linaloongeza uwezekano kwamba mrithi wake ataendeleza sera zake za kimabadiliko, licha ya upinzani mkubwa kutoka kwa wahafidhina.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha