27 Aprili 2025 - 15:51
Ukabidhi wa Hiari wa Silaha Parachinar; Hatua Muhimu kuelekea Amani Endelevu

Baada ya utekelezaji wa Mkataba wa Amani wa Kohat, Waislamu wa madhehebu ya Shia katika wilaya ya Kurram, eneo la Parachinar nchini Pakistan, wamekabidhi silaha zao kwa hiari kwa wawakilishi wa jeshi na maafisa wa serikali ya Pakistan ili kuonesha nia yao ya kutafuta amani.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Kwa mujibu wa "Karam Ashfaq Khan", Naibu Kamishna wa eneo hilo:

  • Mapigano ya umwagaji damu yaliyodumu tangu mwaka jana na kusababisha vifo vya mamia ya watu sasa yanaelekea kumalizika kutokana na hatua chanya zilizochukuliwa na pande zote.

  • Waislamu wa Shia wa Parachinar walikuwa chini ya mzingiro wa kipekee kwa kipindi cha miezi saba iliyopita, na sasa kuna matumaini ya kuvunjwa kwa mzingiro huo.

  • Takribani ngome 1000 zimebomolewa katika eneo hilo na mchakato wa ukusanyaji wa silaha unaendelea katika vijiji vingine vya Parachinar.

  • Pia baadhi ya Waislamu wa Sunni wa Parachinar wamekabidhi silaha zao kwa Serikali ya Pakistan.

Ukabidhi wa Hiari wa Silaha Parachinar; Hatua Muhimu kuelekea Amani Endelevu

Ashfaq Khan alisisitiza kuwa eneo la Kurram linaelekea katika amani ya kudumu na juhudi zote muhimu zinafanyika ili kudumisha utulivu.

Katibu wa Jumuiya ya Husseiniya alikaribisha hatua hiyo, akieleza kuwa ukabidhi wa hiari wa silaha na wakazi wa vijiji vya Parachinar ni hatua muhimu ya kujenga upya imani na kufanikisha amani katika eneo hilo.

Hata hivyo, alisisitiza juu ya umuhimu wa utekelezaji kamili wa vipengele 14 vilivyosalia vya Mkataba wa Amani wa Kohat, na alitaka kufunguliwa kikamilifu kwa barabara za Parachinar ili kumaliza mzingiro wa muda mrefu wa eneo hilo linalokaliwa na Waislamu wa Shia.

Ukabidhi wa Hiari wa Silaha Parachinar; Hatua Muhimu kuelekea Amani Endelevu

Inafaa kutaja kwamba licha ya kutiwa saini kwa mkataba wa amani, bado hali ya usalama katika njia zinazoelekea Parachinar si nzuri, na hivyo misaada ya kibinadamu kama vile dawa na chakula haijafika kwa watu wa Parachinar.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha