Kanali ya Televisheni ya Al Masirah imeripoti kuwa wahamiaji wengine 47 walijeruhiwa, wengi wao wakiwa katika hali mbaya sana, wakati kituo hicho katika jimbo la Saada kikilipuliwa kwa bomu.
Kituo hicho kilichapisha picha zinazoonyesha miili mingi iliyofunikwa kwenye vifusi vya jengo lililoharibiwa.
Lakini shambulio hili lilijiri saa chache baada ya Kamandi Kuu ya Marekani kutangaza kwamba vikosi vyake vimepiga shabaha zaidi ya 800 tangu Rais Donald Trump kuamuru kuimarishwa kwa kampeni ya anga dhidi ya Wahouthi tarehe 15 Machi.
Ilisema mashambulizi hayo "yameua mamia ya wapiganaji wa Houthi na viongozi wengi wa Houthi", wakiwemo maafisa wakuu waliokuwa wakisimamia mipango ya makombora na ndege zisizo na rubani.
Mamlaka zinazoongozwa na Houthi zimesema shambulio hilo limesababisha vifo vya makumi ya raia, lakini wameripoti majeruhi wachache miongoni mwa wanachama wa harakati hiyo.
Licha ya mgogoro wa kibinadamu nchini Yemen uliosababishwa na hujuma ya kijeshi dhidi ya Yemen iliyodumu kwa miaka 11, wahamiaji wanaendelea kuwasili nchini humo kwa boti kutoka Pembe ya Afrika, wengi wao wakiwa na nia ya kuvuka hadi katika nchi jirani ya Saudi Arabia kutafuta kazi.
Badala yake, wanakabiliwa na unyanyasaji, kuwekwa kizuizini, ghasia, na safari hatari kupitia maeneo yenye migogoro, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).
342/
Your Comment