Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu huko Palestina, amesema hayo alipokuwa akielezea hali ya Gaza na kubainisha kwamba, "Siku zijazo huko Gaza zitakuwa mbaya; "Wale ambao hawajauawa kwa mabomu na risasi wanakufa polepole."
Jonathan Whittall, aametoa wito wa kukomeshwa mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza, kufunguliwa kwa njia ya misaada ya kibinadamu, na kuanzishwa tena kwa usitishaji vita.
Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu huko Palestina amesema pia kuwa, licha ya changamoto kubwa, mashirika ya misaada ya kibinadamu yanaendelea kufanya kazi popote yanapoweza kujibu mahitaji ya watu.
Akizungumzia kumalizikaa vyanzo na uwezo mdogo wa mashirika ya misaada katika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, afisa huyo waa Umoja wa Mataifa ameoyesha matumaini kwamba badala ya kuacha historia ihukumu tunataka kuona uwajibikaji wa kweli kwa mgogoro wa sasa.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, baraza la mawaziri la Israel limeidhinisha mswada wa kupiga marufuku kuingizwa misaada yoyote ya kibinadamu huko Ghaza licha ya kwamba Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu yameonya kuwa wananchi wa Gaza wamo kwenye mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha vita vya kikatili vya pande zote dhidi ya ukanda huo, mwezi Oktoba 2023.
342/
Your Comment