Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Katika juhudi za kuratibu na kuwaalika watu mashuhuri wa Kidini na Kiutamaduni wa Tanzania ili kushiriki katika Tamasha la 30 la Kimataifa la Qur'an na Hadithi linaloandaliwa na Jamiatu Al-Mustafa - Dar-es-salaam, Tanzania, Mwakilishi wa Al-Mustafa Dr.Ali Taqavi alifanya ziara katika Ofisi ya Mufti Mkuu wa Tanzania na kukutana naye.
Katika mkutano huo, Bw. Ma’arafi, Mshauri wa masuala ya Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na Dr.Sheikh Al-Hadi Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA) walihudhuria pia.
Washiriki hawa waliohudhuria katika Mkutano huu, kwa pamoja walijadili namna ya kushiriki kwa waandaaji wa mahafali ya Qur'an nchini Tanzania na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Qur'an Tukufu katika Miji tofauti ya nchi hiyo.
Mufti Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Dr Abubakar bin Zubeir, alikaribisha kwa furaha juhudi hii ya Kitamaduni na kusisitiza umuhimu wa programu kama hizi katika kuimarisha mahusiano ya Kidini na Kiutamaduni.
Pia alitoa maagizo muhimu kwa ajili ya ushirikiano wa utekelezaji.
Mkutano huu ulikuwa hatua muhimu katika kukuza ushirikiano wa kitamaduni na wa kidini kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Your Comment