11 Mei 2025 - 15:59
"Wadau wa sekta ya utamaduni wa Afghanistan watilia mkazo juu ya ukarabati wa "Gonbad-e-Begum" / 'Kubba ya Malkia' katika Mkoa wa Ghazni"

"Baadhi ya wadau wa sekta ya utamaduni wa Afghanistan wametilia mkazo umuhimu wa ukarabati na urejeshwaji wa jengo la kihistoria la 'Kubba ya Malkia' katika Mkoa wa Ghazni."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (as) –ABNA– Baadhi ya wadau wa sekta ya utamaduni nchini Afghanistan wametoa wito wa ukarabati na urejeshwaji wa jengo la kihistoria la “Kubba ya Malkia” lililoko katika Mkoa wa Ghazni.

Jengo hili la kihistoria linahusishwa na kipindi cha utawala wa Waghaznawi, na liko katika eneo la Jarm-Toi, katika wilaya ya Jaghatu, umbali wa kilomita 32 kutoka makao makuu ya mkoa wa Ghazni. Ni miongoni mwa alama maarufu za kihistoria nchini Afghanistan.

Kubba hii ya kale ina urefu wa mita 10 na kipenyo cha mita 22. Kwa miaka mingi iliyopita, kutokana na kutopewa uangalizi na ulinzi wa kutosha, imekuwa ikikumbwa na athari za kiasili kama vile mmomonyoko na uharibifu wa mazingira, hivyo sasa inahitaji ukarabati wa dharura.

Mullah Hamidullah Nisar, mkuu wa Idara ya Habari na Utamaduni ya Mkoa wa Ghazni, amesisitiza umuhimu wa ukarabati wa jengo hilo la kihistoria na amesema kuwa atajitahidi kuhakikisha linarejeshwa katika hali yake ya awali.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha