19 Mei 2015 - 13:52
Maporomoko ya ardhi Colombia

Zaidi ya watu 50 wamekufa nchini Colombia, baada ya maporomoko ya ardhi kulikumba eneo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo jana.

Zaidi ya  watu 50  wamekufa nchini  Colombia, baada  ya maporomoko  ya  ardhi  kulikumba  eneo  la  kaskazini  magharibi mwa  nchi  hiyo  jana.

Maafa  hayo  yamesababishwa  na  mvua  kubwa  iliyonyesha katika  eneo  hilo.

Wimbi  la  matope  na  taka taka  viliukumba  mji  wa  Salgar  muda mfupi  kabla  ya  alfajiri. Maafisa  wanasema  hawawezi  kuthibitisha ni  watu  wangapi   bado  hawajulikani  walipo.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos anasema kuwa utawala wa nchi hiyo haujui ni watu wangapi ambao hawajulikani waliko kufuatia maparomoko makubwa ya ardhi ambayo yamewaua zaidi ya watu 50.

Waakazi wa mji wa magharibi wa Salgar wanasema kuwa nyumba wanakoishi watu maskini zilisombwa na matope pamoja na mawe kufuatia mvua kubwa iliyonyesha eneo hilo.

Makundi ya uokoaji yanatafuta kwenye vifusi kujaribu iwapo yatapata manusura.

Rais ameitaja hali hiyo kuwa janga la kitaifa na kusema kuwa atazijenga upya nyumba zilizoaharibiwa.