Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mripuko wa kigaidi umetokea katika hospitali ya Sauli katika mji wa Quetta ambayo ni makao makuu ya wilaya ya Balujestan nchini Pakistan na kupelekea kuuwawa kwa uchache watu 30 na wengine wengi kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa habari wa ABNA aliopo katikia sehemu ya tukio ni kwamba: mripuko huo wa kigaidi umetokea kipindi ambacho wanasheria wa mji huo walikuwa wamekusanyika katika hospitali hiyo wakipinga mauaji ya mmoja kati ya wanasheria wa mji huo ambaye mwili wake ulikuwa umehifadhiwa katika hospitali hiyo, hivyo yawezekana idadi ya waliofariki katika tukio hilo la kigaidi ikaongezeka.
Viongozi wa hospitali ya Quetta wametoa ripoti ya awali nakusema kuwa kutokana na hali ya majeruhi kuwa mbaya, kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka idadi iliotajwa ya waliofariki.
Mpaka sasa hakuna kikundi chochote cha kigaidi kilichotangaza kuhusika na tukio hilo liliotokea leo katika mji wa Quetta nchini Pakistan
mwisho wa Habari/290