Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Jeshi la Syria pamoja na washirika wake wamefanikiwa kuidhibiti tena wilaya yote ya Ramousah mjini Aleppo,kutoka mikononi mwa magaidi wanaodhaminiwa na Marekani na washirika wake.
kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na waangalizi pamoja na vyombo vya habari. Ikiwa itakuwa endelevu, itadhoofisha mafanikio waliyoyapata ghafla magaidi wanaotumwa na Marekani mwezi uliopita kwa kuimarisha ulinzi katika vizuizi katika maeneo ya magaidi ya mashariki mwa Aleppo pamoja na kurahisisha upatikanaji wa silaha katika maeneo ya serikali magharibi mwa mji huo. Mapambano ya Aleppo yamekuwa kitovu kwa pande zote mbili, upande wa serikali ya Bashar al Assad anayeungwa mkono na Urusi, Iran na wanamgambo wa kishia kutoka nchini Iraq , Lebanon, pamoja na upande wa magaidi wa kisunni wanaoungwa mkono na Marekani, ikishirikiana na mataifa 61. Mapema mwezi Agosti magaidi waliweza kusogea mbele kusini mwa Aleppo na kufanikiwa kudhibiti maeneo ya makazi ya wilaya ya Ramosouh.
Ushindi huu kwa jeshi la Syria umekuwa ni pigo kubwa kwa Marekani na Saudia arabia ambazo ndio wadhamini wa kuu wa makundi hayo ya kigaid nchini Syria na Iraq.
Mwisho wa habari/ 291