30 Mei 2025 - 22:18
Source: Parstoday
Rais Pezeshkian: Silaha za nyuklia hazina nafasi katika doktrini ya Jamhuri ya Kiislamu

Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesisitiza kuwa, Iran kamwe haitaacha haki yake ya kisheria ya kurutubisha madini ya urani.

Daktari Pezeshkian amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, katu Iran haitaacha kurutubisha madini ya urani kwa madhumuni ya matibabu, uchunguzi wa magonjwa, afya, kilimo na viwanda na kueleza bayana kwamba, silaha za nyuklia hazina nafasi katika mafundisho na itikadi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika ziara yake nchini Oman, Rais Masoud Pezeshkian wa Iran alifafanua katika mahojiano na televisheni rasmi ya nchi hiyo kuhusu masuala ya pande mbili kati ya nchi hizo mbili, pamoja na maslahi ya kieneo na kimataifa ya Iran na Oman na masuala muhimu zaidi ya hivi sasa duniani.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameweka ujumbe katika mtandao wa kijamii wa X kwa lugha ya Kiajemi na Kiarabu, alipokuwa akirejelea safari yake ya siku 2 huko Muscat, mji mkuu wa Oman na kuandika: Katika safari hiyo ya Oman, alipokuwa akikutana na kuzungumza na ndugu yangu Sultan Haitham bin Tariq, hati 18 zilitiwa saini kati ya nchi hizo mbili na nyaraka za ushirikiano.

Katika mazungumzo na runinga ya Oman, Rais Pezeshkian alisema: “Tuko kwenye maelewano ya hali ya juu kisiasa, na mikutano yetu ya pamoja ilifanyika kwa mitazamo iliyowiana.

Katika masuala yote ya kieneo, ukiwemo mtazamo kuhusu Palestina, Gaza na masuala yanayohusiana na amani na utulivu katika eneo hili, kuna uratibu na ulinganifu mkubwa wa mitazamo kati ya Oman na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hivyo tuna mafungamano mazuri katika ngazi ya kisiasa, amebainisha Rais Pezeshkian.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha