Kulingana na Shirika la Habari la AhlulBayt (ABNA), kiongozi wa Wakatoliki duniani, kuhusu hali mbaya na mauaji ya kimfumo yanayofanywa na utawala wa Kizayuni katika eneo hilo, alisema: "Ninafuatilia kwa wasiwasi mkubwa hali mbaya sana ya kibinadamu huko Gaza. Watu wa Gaza wanakabiliwa na ghasia na vifo kutokana na njaa."
Robert Provost, pamoja na kutoa wito wa kusitishwa mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kizayuni, pia alitoa wito wa kuruhusu upatikanaji usio na masharti wa misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza.
Maneno haya ya Papa Leo XIV yalitolewa wakati wa sala yake ya kawaida ya Jumapili kutoka dirishani mwa ofisi yake inayoelekea Uwanja wa Mtakatifa Petro, ambapo alizungumzia hali ya Ukanda wa Gaza.
Kulingana na takwimu za hivi punde kutoka Wizara ya Afya ya Gaza, zilizotolewa Jumapili, idadi ya vifo vinavyotokana na njaa na utapiamlo tangu Oktoba 7, 2023 imefikia Wapalestina 133, ikiwemo watoto 87.
Hali mbaya ya maafa huko Gaza, huku kukiwa na ukimya wa jumuiya za kimataifa na kutochukuliwa hatua na taasisi za haki za binadamu, na kwa matamshi yasiyo na tija tu na kuonyesha huruma kwa mateso na maumivu ya wanawake na watoto wa eneo hili, inaendelea kuongezeka kila siku.
Your Comment