Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo asubuhi, Makamu wa Kwanza wa Rais alifanya ziara bila kutangazwa kwenye kituo cha amri cha Shirika la Kitaifa la Huduma za Moto na Dharura na Jumuiya ya Hilali Nyekundu.
A'rif: Leo, hatutaruhusu tena kujadiliana juu ya urutubishaji wa madini ya uranium ndani ya eneo la nchi yetu.
Nia ya maadui ya kuporomoka kwa jamii (ya Iran) iligeuzwa kuwa mafungamano ya kijamii na uwepo (na uthabiti) wa watu wa Iran.
Iran haitafuti vita, lakini lazima tujitayarishe kikamilifu kwa ajili ya ulinzi na kujihami.
Badala ya kila mwanasayansi aliyeuawa kishahidi, vijana kadhaa na wenye nguvu zaidi watakuja mbele (na kuendeleza harakati zile zile uwanjani). Makao makuu ya ujenzi na ukarabati yataundwa kwa msaada wa watu na mashirika yasiyo ya kiserikali na ya kutoa misaada. Ninashukuru hima na juhudi za mashirika ya usaidizi katika siku 12 za vita zilizopita.
Your Comment