Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ebrahim Rezaei, msemaji wa Tume ya Usalama ya Kitaifa ya Bunge, katika mahojiano na kituo cha Habari za Haraka amesema:
Sasa, zaidi ya siku 10 baada ya kuanza kwa mzozo wa vita, Israeli imefikia hitimisho kwamba uwezo na nguvu za Wairan haziwezi kupingwa na imejutia vita na Iran.
Mashambulizi dhidi ya Lebanon na Syria na mauaji ya viongozi wa Hizbullah yaliufanya utawala wa Kizayuni uamini kwamba, unaweza kuiangamiza Iran kupitia hatua za kijeshi na hatimaye kwa kuanzisha ndani ya Iran maandamano ya mitaani, na kuiweka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika wakati mgumu, jambo ambalo halikuwa na badala yake likawa jambo jingine tofauti kabisa na ilivyokuwa dhana yao.
Sasa Israel imebakia kujutia na kujilaumu kuingia vitani na Iran na kukiri kuwa Nguvu ya Iran sio rahisi kuikabili. Hii ni baada ya kupata Mashambulizi makali zaidi ya Makombora ya Iran yenye uharibifu mkubwa na milipuko ya kutosha katika kila kona ya Utawala Ghasibu wa Israel.
Your Comment