Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA likinukuu mtandao wa Al-Masirah, Abdul Wahid Abu Ras, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya Sanaa, katika mahojiano na shirika la habari la Saba la Yemen, alitangaza: "Tangazo la adui Mwisraeli la kuitambua Somaliland kama nchi huru ni sehemu ya mpango wa Kizayuni unaojulikana kama 'Mashariki ya Kati Mpya'."
Aliongeza: "Mipasuko na mianya ambayo adui Mzayuni anaitumia kupenya katika kanda hiyo ni matokeo ya sera za utegemezi za baadhi ya serikali za Kiarabu."
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali iliyopo Sanaa alibainisha: "Marekani ni mshirika katika njama hii, na matamshi yanayotolewa siku hizi si lolote bali ni mgawanyo wa majukumu na utawala wa Kizayuni."
Abu Ras pia alisisitiza: "Kutosheka kwa serikali za Kiarabu na kutoa taarifa tu, ni kukwepa majukumu na ni aina fulani ya ushirikiano ili mipango ya Kizayuni itekelezwe."
Mwishoni alionya: "Kanda ya Kiarabu inakabiliwa na uingiliaji mkubwa na miradi ya migawanyiko kutokana na ushirikiano huu wa fedheha wa serikali nyingi za Kiarabu ambazo zinabeba dhima kamili."
Your Comment