28 Desemba 2025 - 08:55
Source: ABNA
Upinzani mkali wa Venezuela dhidi ya hatua ya Netanyahu kuitambua Somaliland

Wizara ya Mambo ya Nje ya Venezuela imesema katika taarifa yake: "Tunasisitiza utambuzi kamili na usio na masharti wa Caracas wa mamlaka, umoja na ukamilifu wa ardhi ya Somalia."

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA likinukuu shirika la habari la Al Jazeera, Wizara ya Mambo ya Nje ya Venezuela leo Jumamosi imesema katika taarifa yake: "Tunasisitiza tena utambuzi kamili na usio na masharti wa Venezuela wa mamlaka, umoja na ukamilifu wa ardhi ya Jamhuri ya Shirikisho la Somalia."

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Venezuela imeelezwa kuwa: "Caracas inazingatia maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika ambayo yanaheshimu ukamilifu wa ardhi ya Somalia, na inayaunga mkono."

Gideon Sa'ar, Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni, alitangaza siku ya Ijumaa kuwa utawala huo na Jamhuri ya Somaliland wametia saini makubaliano ya kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na kuteuliwa kwa mabalozi na kufunguliwa kwa balozi. Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, hapo awali katika mazungumzo ya video na Abdirahman Mohamed Abdullahi, kiongozi wa wanaotaka kujitenga wa Somaliland, alimwalika kutembelea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Vyombo vya habari vya utawala ghasibu hapo awali vilikuwa vimeitaja Somaliland kama chaguo mojawapo la utawala huo kwa ajili ya kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina wanaoishi Gaza kutoka nchi yao ya asili. Wanaotaka kujitenga wa Somaliland walitangaza uhuru wao kutoka Somalia mwaka 1991 lakini hadi sasa hakuna nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa iliyowatambua. Wanashikilia sehemu ya kaskazini ya Somalia.

Your Comment

You are replying to: .
captcha