4 Januari 2026 - 10:54
Muundo Mpya wa Ukuta wa Uwanja wa Palestina Tehran Wabeba Ujumbe Mkali wa Kiebrania katika Kumbukumbu ya Shahid Soleimani | Mnazidi kukaribia kutoweka

Katika kumbukumbu ya shahidi Jenerali Qasem Soleimani, jadariya jipya katika Uwanja wa Palestina, Tehran, limeibuliwa likiwa na ujumbe wa Kiebrania unaobeba onyo la kiishara kuhusu kukaribia mwisho wa zama za ubeberu na uvamizi, likisisitiza kuendelea kwa njia ya mapambano na msimamo wa upinzani.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Muundo mpya wa uchoraji wa ukutani (jadariya) katika Uwanja wa Palestina katikati ya mji mkuu wa Iran, Tehran, umewekwa hadharani sambamba na kumbukumbu ya mwaka wa kuuawa Shahidi Jenerali Qasem_Soleimani. Ujumbe ulioandikwa kwa lugha ya Kiebrania unasema: “Kila siku mnazidi kukaribia saa ya kutoweka.”

Ujumbe huu wa kiishara unaakisi msimamo wa mhimili wa mapambano na kusisitiza kuendelea kwa njia na fikra za shahidi Soleimani katika kukabiliana na ubeberu na uvamizi.

Uchoraji huu ni sehemu ya mfululizo wa kazi za kisanaa zinazobeba ujumbe wa kisiasa na kitamaduni, huku ukihifadhi kumbukumbu ya viongozi wa mapambano kama alama ya kusimama imara na uthabiti.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha