Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Sayyid Ali Khomeini alisema kuwa utawala wa Kizayuni ni ngome kuu ya Marekani katika eneo, na kama mataifa ya Kiislamu yangekuwa na uwezo, yangefanya kwa Israel yale ambayo Hamas ilifanya tarehe 7 Oktoba 2023.
Akasema:
“Lengo la Israel katika vita dhidi ya Iran ni moja tu: kuigawa Iran.”
Ameongeza:
“Kwa mtazamo wangu, vita kati ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ni jambo la mbali sana. Lakini kama vita vitatokea, hatutaogopa, tutapambana na tumeonyesha uwezo wetu. Marekani na Israel wameifanya dunia iwe kama msitu wa wanyama; kutofautisha kati yao haina maana.”
Wasiwasi upo, lakini hofu hapana
Akijibu swali kuhusu mustakabali wa Mapinduzi, alisema:
“Ndiyo, nina wasiwasi, lakini siogopi. Wasiwasi ni wa kawaida kwa anayekipenda kitu anapokiona kipo hatarini. Lakini hofu mbele ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu hapana. Njia yetu mwanzo wake ni kujitoa mhanga na mwisho wake ni shahada, na hakuna kushindwa ndani yake.”
Mataifa ya Kiislamu yakipata uwezo yatafanya kama Hamas
Sayyid Ali Khomeini alisema:
“Njia pekee ya maisha yetu ni mapambano ya kusimama imara. Tuko katika vita vya uwepo. Israel na Marekani wanajua kuwa siku ambayo mataifa ya Kiislamu yatakuwa na uwezo wa kuishambulia Israel, watafanya hivyo. Leo baadhi hawafanyi kwa sababu hawana uwezo.”
Israel inalenga kuigawa Iran
Akasema:
“Sera ya hakika ya Marekani na Israel ni kuidhoofisha eneo. Israel ikipata nafasi, itazuia maendeleo ya kiuchumi ya Waislamu. Wanataka kuigawa Iran kama ilivyogawanywa Dola ya Ottoman. Iran kubwa ikigeuzwa nchi ndogo ndogo, kila nchi itahitaji Israel, na Israel itasema: ‘piga’, nao watasema: ‘Ndiyo bwana’. Ndiyo maana tulichagua njia ya upinzani.”
Israel ni kambi kubwa ya kijeshi ya Marekani
Sayyid Ali Khomeini alisema:
“Marekani imemchagua Israel kuwa kambi yake kubwa zaidi ya kijeshi. Kutenganisha Marekani na Israel hakuna maana. Marekani daima husimama upande wa Israel.”
Vita na Marekani ni mbali, lakini tukilazimishwa hatuogopi
Alisema:
“Madhalimu huongea kwa lugha ya nguvu. Amani kati ya dhalimu na dhaifu haiwezekani. Uchambuzi wangu ni kuwa vita ni mbali, lakini vikija, hatutaogopa. Tulirusha makombora, yakapiga shabaha na yakaharibu. Huo ni ujumbe wetu kwa istikbari.”
Leo mtu maarufu zaidi Iran ni Ayatollah Khamenei
Sayyid Ali Khomeini alisema:
“Kwa mujibu wa tafiti, leo mtu maarufu na mwenye nguvu zaidi Iran ni Ayatollah Ali Khamenei. Anaunganisha nguvu na umaarufu.”
Akaongeza kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ana: Uchamungu na imani ya kweli, uelewa wa kihistoria, kimkakati na kijiografia, uzoefu wa zaidi ya miaka 50 katika siasa na mapambano, na ushujaa wa asili.
Akasema:
“Akiwa amesema jambo litatokea, karibu kila mara hutokea.”
Kumbukumbu yake na Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah
Sayyid Ali Khomeini alisimulia kuwa Sayyid Hassan Nasrallah aliwahi kutembelea nyumba ya Imam Khomeini huko Jamaran akiwa na Shahidi Qassem Soleimani na Imad Mughniyah.
Alipopewa kitambaa cha Imam Khomeini kama zawadi, Nasrallah alilia na kusema:
“Nyumba yangu iliharibiwa vitani, sikuhuzunika. Lakini nilihuzunika kwa kupoteza zawadi ya Imam. Leo Imam amenipa tena kitu kutoka kwake.”
Akasema:
“Nasrallah alikuwa mtu wa jihadi, mantiki na uhalisia. Leo vijana wa Umma warejee maneno yake. Mashahidi wako hai.”
Busara ya watu wa Iraq
Kuhusu Iraq alisema:
“Watu wa Iraq wameonyesha basira. Karibu wabunge wote wanapenda Uislamu wa kweli. Na leo, Ayatollah Sayyid Ali Sistani ndiye mtu mwenye ushawishi mkubwa zaidi Iraq. Uwepo wake ndio unaolinda uthabiti na umoja wa Iraq.”
Tunatetea haki yetu
Mwisho alisema:
“Hatuwaogopi. Tunatetea haki yetu na nchi yetu. Kwa mapenzi ya Mungu vita havitatokea, lakini vikitokea, tumesimama mizizi hapa. Marekani hawataona kudhalilishwa kwa Iran. Tulipitia vita vya siku kumi na mbili na adui alidhani tutaporomoka, lakini kinyume chake kilitokea.”
Your Comment