Harakati ya Hamas imesisitiza kuwa: Mwenge wa “Dhoruba ya Al-Aqsa” utaendelea kuwaka daima, ukiwapulizia roho ya kusimamia haki, misingi, na umoja wa kitaifa. Moto wake katika nyoyo za taifa letu kubwa hautazimika kamwe, ijapokuwa kujitolea ni kwa gharama kubwa na nguvu za adui ni nyingi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, huku akishukuru msimamo wa uwajibikaji wa Pakistan katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kupinga matumizi mabaya ya nchi tatu za Ulaya, alisisitiza kwamba Azimio namba 2231 lazima, kwa mujibu wa masharti yake na maandiko ya makubaliano ya nyuklia (JCPOA), lichukuliwe kuwa limekamilika katika muda uliopangwa, yaani tarehe 26 Mehr 1404 (18 Oktoba 2025).