Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna -; "Benyamin Netanyahu", Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Kizayuni ametangaza hofu ya kuwepo makundi ya Muqawamah katika Ukanda wa Gaza na kusema. Kuendelea kuwepo kwa Hamas huko Gaza kutamaanisha kushindwa kwa Israel na kujengwa upya kwa mhimili wa Iran.
Netanyahu amesema kuwa video hiyo iliyotolewa na Hamas ya mateka ni sehemu ya vita vya kisaikolojia vya kundi hilo na ni vigumu kuitazama.
Alidai kuwa picha hizi zimeimarisha azma yake ya kuwarudisha wafungwa (mateka) kutoka Gaza.
Netanyahu alidai kuwa atasababisha kuachiliwa kwa wafungwa wa kizayuni kutoka Gaza kwa kupitia shinikizo la kijeshi na kisiasa kwa wakati mmoja.
Kama ilivyokuwa hapo awali, Netanyahu aliahidi jambo moja tu la kupelekea kuwaachilia kwa wafungwa wote kwa kizayuni kutoka Gaza na kuharibu kabisa harakati ya Hamas, bila kuchukua hatua yoyote ya kivitendo na kupitia kuvuruga mchakato wa kubadilishana wafungwa baina ya Isarel na vikundi vya mapambano ya Muqawamah (upinzani).
Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni alidai: Iwapo Hamas itasalia Gaza, (matukio) visa zaidi vya kutekwa Wazayuni vitatokea na shambulio la Oktoba 7 litarudiwa.
Your Comment