4 Novemba 2026 - 11:28
Uwepo wa Uturuki usio na uhalali kaskazini mwa Iraq licha ya makubaliano ya kuondoa vikosi vyake

Luqman Hassan, mwanachama wa Harakati ya Ukombozi wa Wakurdi, amesisitiza kuwa kuendelea kwa uwepo wa kijeshi wa Uturuki kaskazini mwa Iraq ni kukwepa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Ali al-Zaidi, Waziri Mkuu wa Iraq, na Recep Tayyip Erdoğan, Rais wa Uturuki, kuhusu kuondolewa kwa vikosi vya Uturuki kutoka kaskazini mwa Iraq.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Luqman Hassan, mwanachama wa Harakati ya Ukombozi wa Wakurdi, amesema kuwa kuendelea kwa uwepo wa kijeshi wa Uturuki kaskazini mwa Iraq kunakiuka makubaliano yaliyofikiwa kati ya Baghdad na Ankara.

Katika mahojiano na shirika la habari la Al-Maaloumah, alisema kuwa mwaka 2024 kulitokea mapigano kati ya Chama cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) na upande wa Uturuki. Hata hivyo, mwishoni mwa mwaka huo, Abdullah Öcalan, kiongozi wa PKK, alitangaza mpango wa kusitisha mapigano, kuvunjwa kwa chama hicho na kumaliza shughuli zote za kijeshi.

Aliongeza kuwa tangu wakati huo, hakuna tena sababu ya kuendelea kuwepo kwa vikosi vya Uturuki kaskazini mwa Iraq.

Luqman Hassan alisema kuwa vikosi vya Uturuki vinaendelea kuwepo bila uhalali katika Mkoa wa Kurdistan na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Nineveh. Alisisitiza kuwa hakuna tena tishio kutoka kwa PKK dhidi ya serikali ya Uturuki, kwa kuwa Öcalan amekitaka chama hicho kuweka chini silaha.

Alifafanua kuwa kuendelea kwa uwepo wa Uturuki kaskazini mwa Iraq kunathibitisha, kwa mtazamo wake, kuwepo kwa nia ya kutwaa baadhi ya maeneo ya ardhi ya Iraq.

Haya yanajiri licha ya kuwepo kwa makubaliano kati ya Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia al-Sudani? na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, kuhusu kuondolewa kwa vikosi vya Uturuki nchini Iraq.

Hassan alihitimisha kwa kusema kuwa kuendelea kwa vikosi hivyo kaskazini mwa Iraq ni kukwepa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Baghdad na Ankara, hususan baada ya kuondolewa kwa sababu iliyokuwa ikitumika kuhalalisha uwepo wa vikosi vya Uturuki katika eneo hilo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha