Ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Halah Fakhir Mcheza Sinema wa Misri alichagua kuvaaa Hijabu na kusema:miezi 3 nikuwa na fikiria kuvaa Hijabu na sasa nimeweza kufikia katika lengo langu na kuzidi Rizki kwa sababu ya Hijabu.
Akiendelea kusema:kuvaa kwangu Hijabu nilikuwa napewa kazi nyingi na nafasi za kuchezaTamthilia na Sinema.
Mcheza Sinema huyu alijibu baadhi ya Waandalizi wa Sinema ambao wapo dhidi ya Uislamu kusema;Ujira wangu wa Dunia na Akhera baada ya kuvaa Hijabu umezidi kuliko hapo kabla.
Halah Fakhir alizaliwa Mwaka 1946 katika Mkoa wa Iskandariyah na kuanzia Mwaka 1960 hadi sasa alishiriki katika Tamthilia na Sinema 139.
Kutokana na ripoti ya Miaka iliyopita hasa katika muamko wa Kiislamu wa Misri kutokana na ufisadi uliofanyika Wananchi walikasirika na Wanawake kukimbilia Hijabu kuwa hifadhi, pia kabla Halah Fakhir Hanan Tark Mchezaji wa Sinema Maarufu alichagua vazi la Hijabu kuwa vazi lake.