Kila siku twapata ripoti tofauti kunako Wanawake wa Rusia hasa katika Mkoa Kazan kwa kuvaa kwao vazi la Kiislamu kila waendapo.
Alisa Husainova ni maarufu katika Nchi ya Rusia hasa katika Mkoa wa Kazan, Mkoa ambao ni mashuhuri Rusia kwa vivutio vya utalii.
Mwana Musiki huyo katika mwaka wa 2000 aliweka mkataba na timu za Moskow kwa kufungua hafla kwa Muziki, hilo lilisababisha kuongeza umaarufu wa Mwana Muziki huyo na kufahamika katika bara la Ulaya, na Mwandishi wa Rusia Artemi teroitski alimpa jina la Mfalme wa Muziki Nchi Rusia.
Katika mwaka wa 2004 alitoa albam mpya ya Muziki na kuwa albam bora ya mwaka huo Nchini Rusia, Mwana Muziki huyo pia alikwisha itishwa sehemu tofauti ili kudumbwiza watu km Nchi ya Swiss na Stonia, pia Mwana Muziki huyo hakuridhika na umaarufu wake bali alichukua hatua ya kuacha kuimba Muziki na kuchagua hijabu kuwa vazi lake.
Familia ya Alisa Husainova ni Waislamu, Mme wake aitwa Ahmad na Kaka yake ni Bulat, na Mama yake alikwishasoma katika Shule ya Muhammadiah katika Mkoa wa Kazan Rusia.
Alisa amesema: Matarajio yangu ni kuwa Mwana Muziki na Mama bora, kuwa Mwana Muziki nilifaanikisha ila kuwa Mama bora kamwe sikufaanikisha na sikuweza kuwa Mama bora kwa sababu hii; Dunia ya leo akina Mama walokuwa wengi hawalei Watoto wao kwa sababu zao km kufanya kazi na kutokuwa na muda wa kulea Watoto hilo la sababisha kuajiri mlezi wa Watoto (House Girl) kwa muda ambao hatokuwepo nyumbani.
Akiendelea kusema: mara nyingi nilikijiuliza kwanini nimeweza kuwa Mwana Muziki bora na sikuweza kuwa Mama bora?! Swali hilo lilinipelekea kuwacha kuimba Muziki ili niwe Mama bora, na kuacha kwangu kuimba Muziki niliweza kuwa Mama bora kwa kiwango fulani.
Akimalizia kwa kusema: Nadharia yangu ni kwamba ni lazima kwa kila mtu kutafuta njia ya kuingia peponi na sidhani km kuna njia bora km hii niliochagua.
Mama huyo pia alieleza kuwa apenda Kijiji cha Starotatarsky mbacho kipo katika Mkoa wa Kazan Nchini Rusia.
Alisa Husainova sasa muda wake mwingi autumia kwa Mtoto wake Mariam na kuwa Mama bora wa Mkoa wa Kazan na kuhisi kuwa kiungo muhimu wa Familia yake, pia sasa ajihisi kuwa mtulivu na kuridhia maisha yake ambapo hapo kabla hakuwa akijihisi majukumu ya aina yoyote ile, kwani lengo lake lilikuwa ni umaarufu tu.
Ripoti hii imetolewa na Bwana Danic Garaev katika Tovuti ya Islamnews.