Kwa Jina la Mwenyezi Mungu,Mwingi wa Rehema,Mwenye Kurehemu
Asalaam alaykum.
Hivi sasa umefika wakati wa kuichunguza hadithi wanayoitegemea Mawahabi kuharamisha kujenga juu ya makaburi.Kabla ya yote tunaitaja hadithi yenyewe kwa sanadi aliyoipokea Muslim ktk kitabu chake:
"Ametusimulia Yahya ibn Yahya,na Abubakar ibn Abi Shaiba na Zuhayr ibn Harb,Yahya ametusimulia;(na watu wawili wa mwisho wamesema):Ametusimulia Waki'i, amepokea kutoka kwa Sufyan,toka kwa Habib bin Abi Thabit,nae kapokea kwa Abi Wai'l ambae kapokea toka kwa Abil Hayyaj Al Asad amesema:
"Ali ibn Abi Talib aliniambia:Je,nikutume kwa jambo ambalo Mtume wa Mwenyezi Mungu alinituma kwamba,usiache sanamu yoyote ila uiondoshe wala kaburi lolote lile lililonyanyuka isipokua ulisawazishe"[Tazama:
1)Sahih Muslim Juz 3 kitabul-Janaiz uk 612,
2)Sunan Tirmidhi Juz 2 uk 256 Babu Majaa fi taswiyatil-qubur
3)Sunan An-nasaiy Juz uk 4 uk 88 Babu Taswiyatil-qubur

SASA TUICHAMBUE HADITHI HIYO:
Kwa ujumla tunapotaka kutoa ushahidi kwa kutumia hadithi ili tutoe hukmu miongoni mwa hukmu za Mwenyezi Mungu,hapana budi hadithi hiyo itimize masharti haya mawili:
1)KUSIHI KWA SANADI:
Hii ikiwa na maana kwamba,WAPOKEZI na WATU WAHUSIKAO kwenye hadithi yenyewe,ktk kila ngazi wawe ni waaminifu kiasi ambacho IWEZEKANE kuwategemea ktk maneno yao.
2)USHAHIDI WA HADITHI:
Maana yake ni kwamba,matamko na sentensi zilizomo ktk hadithi hiyo ziwe zimetimia ktk kuelekeza makusudio yetu kwenye hadithi hiyo,kiasi waweza kuifahamu na wengine wanaofahamu vizuri lugha iliyomo ktk hadithi hiyo,na wazifahamu pia kanuni zake kama tunavyozifahamu sisi na waweze kutoa matokeo tunayoweza kuyatoa.

Na kwa bahati nzuri,hadithi hii ya Abul-Hayyaj IMEKOSA sharti zote mbili na hasa ile ya pili,kwani hakuna mahusiano yoyote kabisa ya kujenga juu ya makaburi.
SASA TUNAANZA UFAFANUZI:
A)Ama kwa upande wa Sanad,ndani ya hadithi hii wamo wapokezi ambao,wanachuoni wa hadithi hawakuafikiana juu ya uaminifu wa wapokezi hao,na hapa chini tunataja majina ya wapokezi waliomo ktk hadithi hii ambao wanachuoni wa hadithi wamezikataa hadithi zao:

1)Waki'
2)Sufiyan Ath-Thauri
3)Abu Wai'l Al Al-Asadi

Wapokezi hawa wanne amewatia kasoro Al-Hafiz ibn Hajar Al-'Asqalani ktk kitabu chake kiitwacho "Tahdhibut-Tahdhib" na amewataja kwa sifa ambazo zinaondoa uaminifu ktk hadithi yao hii tuliyoitaja hapo juu na pia kwenye hadithi nyingine.

(1)Kwa upande wa huyu Waki' amepokea Al-Hafiz Al-Asqalani kutoka kwa Ahmad bin Hanbal[huyu ni Imam wa Madhehebu ya Kihanbal] amesema:
"Hakika Waki' amefanya makosa ktk hadithi mia tano"[Tazama:Tah-dhibut-Tahdhib Juz 11 uk 125]

Anasema tena Al-'Asqalani akimnakili Muhamma bin Nasr Al-Marwazi:
"Waki' alikua akisimulia hadithi kwa mujib wa maana yake,isitoshe hakua mtaalam wa lugha"[Tazama:Tah-dhaibut-Tah-dhib Juz 11 uk 130]

(2)Kwa upande wa Sufyan At-Thauri
Al-Asqalani anasema kwa kumnakili ibn Mubarak:
Sufiyan alikua akisimulia hadithi,basi mimi nikafika kwake na yeye alikua anafanyia Tadlis hadith hiyo(kufanya udanganyifu ktk hadithi)basi aliponiona aliona haya(kwa tendo lake hilo)[Tazama:Tah-dhibut-Tahdhib Juz 4 uk 115]

Kitendo cha kudanganya ktk hadithi kwa namna yoyote ile,kinajulisha kwamba msimuliaji hana uadilifu na ukweli,kwa hiyo alikua anakifanya kitu kisicho cha ukweli,kionekane kua ni kweli,kama ilivyo maana ya tadlis ktk lugha ya Kiarabu.
(3)Ama huyu "Habib ibn Abi Thabit",Al-Asqalani ameandika akimnakili Abu Habbani:
"Kwa hakika Habib Alikua mdanganyifu"[Tazama:Tah-dhibut-Tah-dhib Juz 2 uk 179]
(4)Ama huyu Abu Wa'il Al-Asad,yeye alikua mpinzani wa Imam Ali(a.s) na ni miongoni mwa watu waliomfanyia uadui na kero Imam Ali(a.s)[Tazama:Sharh Nahjul-Balagha ya Ibn Abil-Hadid Juz 9 uk 99]
Hawa ndio wanaotegemewa na Mawahabi.Mwenyezi Mungu anasema:"Hakika wanaozua uwongo ni wale wasioziamini aya za Mwenyezi Mungu;na hao ndio waongo"(Qur'an 16:105).Mawahabi wanawategemea "wale wasioziamini aya za Mwenyezi Mungu"Jee "wale wasioziamini aya za Mwenyezi Mungu...." ni Waislam???Na wale wanaowategemea watabaki Waislam??