Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Sheikh Abdurahman Ibn Nasir Al-Baraak mufti maarufu wa Saudia Arabia aliandika katika ukurasa wake wa Twiter: Kutegemea mfumo wa uchaguzi kwa ajili ya kuchagua wagombea wa urais wa jamuhuri ni haramu.
Sheikh aitakidi: Kuchagua kila Kiongozi kwa ajili idara za Waislamu ni wadhifa wa WATATUZI WA MAMBO NA MAULAMAA na si kwa kila Muislamu au watu wa kawaida, Uchaguzi ni mfumo wa kifisadi ambao Waislamu, Sheria ya Kiislamu na akili haijathibitisha kutumiwa mfumo huo na hiki ni kitu maadui wa Uislamu waliingiza katika fikira za Waislamu.
Kutumia mfumo wa uchaguzi ni kujishabihisha na makafiri, Uchaguzi umejawa na uongo, Ahadi za uongo na kuiba kura za watu, Na hii dalili tosha ya kuharamisha uchaguzi.
Sheikh Abdurahman Ibn Nasir Al-Baraak ni mmoja ambae aitakidi kua lazima Kaaba ivunjwe na kujengwa namna nyengene ambayo itakua haiwezekani kukusanyika Wanawake na Wanaume sehemu moja, Aidha aitakidi kua Wanawake wanaoomba leseni za udereva Saudia Arabia waskahiki kifo.