Ashukuriwe allah mwingi wa rehema mwenye kurehemu, ziada na rehema na amani ziwe juu ya kipenzi chake Mtukufu Mtume Muhammad(S.A.W.W) na watu wa nyumbani kwake watukufu.
Haya ni majibu muhtasari kwa walokuja tuhumu na kuongelea suala ambalo ni nyeti katika pande mbili(Mashia na Masunni) kwa madai ya kua Mashia wapambia batili kuwa haki!!.
Majibu ya vipeperushi vilosambazwa tutajibu kama ifuatavyo:
1-Mashia waitakidi kuwa Imam Ally(AS) ni maasum, yaani hafanyi kosa kubwa wala kosa dogo, lengo la maneno haya ni kwamba; Kila alobeba majukumu ya Mtukufu Mtume(S.A.W.W) lazima awe ni maasum kwa kuwa yeye ndiye alochukua nafasi yake(S.A.W.W) baada yake, akili ya hukumu kuwa kila Nabii lazima awe maasum kulingana na ujumbe na mzigo alobeba Nabii huyo, vivyo hivyo akili yakubali kuwa ataechukua nafasi hiyo lazima awe kama yeye. Kama upande wa Sunni wanapinga kuwa anaekuja baada ya Mtume atakiwi kuwa na sifa kama za mtume basi upande washia sivyo hivyo.
2-Suala la kumuozesha Imam Ally(AS) Mtoto wake Ummu Kulthum kwa Omar(RA) itajibiwa kwa nukta mbili zifuatazo;
1-WAPOKEZI WA HADITH WANAMATATIZO YA UPOKEZI.
1- Walopokea hadith hii upande wa Masunni ni; IBN SAAD(TABAQATUL KUBRA, JUZ 8, UK 462.) ALKHATIB ALBAGHDADI(TARIKHUL BAGHDADI, JUZ 6, UK 182.) IBN ATHIR(USUDUL GHABA, JUZ 5,UK 614) IBN HAJAR AL-ASQALANI(AL-ISABA, JUZ 4, UK 492.) na wengine wengi kama HAKIM NAISHABURI, BAIHAQI NA IBN ABDULBAR na...
2- La ajabu ni kwamba SAHIH BUKHARI NA SAHIH MUSLIM hadith hii haikupokelewa, na kuna baadhi ya hadith kwa kuwa hazipo ndani ya vitabu hivyo(SAHIH BUKHARI NA SAHIH MUSLIM) hupingwa, aidha MUSNAD AHMAD NA MUSNAD IBN ABII YAALAA haikupokelewa!!! Pia Vitabu SITA SAHIHI kwa upande wa Masunni haikupokelewa hadith hii.
3- BAIHAQI asema wapokezi wa hadith hiyo ni MADHAIFU HAWAKUBALIWI HADITH ZAO, REJEA TAHDHIBU TAHDHIB JUZ 11, UK 382, JUZ 1, UK 44, JUZ 8, UK 27, JUZ 4, UK 106. Na vitabu vyengine kama; MIZANUL ITIDAL JUZ 4,UK 334, TARIKHUL BAGHDADI JUZ 13, UK 472, WADHOOFISHA WAPOKEZI WA HADITH HIYO.
2-MANENO YA HADITH.
1- Watu waliposikia kuwa Omar(RA) ataka kumuowa Mtoto wa Ally(AS) walishangaa na Omar(RA) aliwajibika kuwaeleza watu lengo la kumuowa Binti huyo kwa kusema: NILIMSIKIA MTUKUFU MTUME(s.a.w.w) AKISEMA: KILA KIZAZI KITATOWEKA ISIPOKUA KIZAZI CHA HUYU AKIASHIRIA KWA ALLY(AS). Hii ndiyo sababu ya kwanza kutaka kumuowa Binti wa Ally(AS).
2- Katika hadith hiyo pia yaeleza kuwa Ally(AS) alitowa udhuru kwa Mtoto wake kuwa bado ni mgodo, na kueleza kuwa binti yake yupo tayari kwa ajili ya Watoto wa Jaafar(RA).
3- Baadhi ya wapokezi wa hadith waeleza kwamba: IBN SAAD NA KHATIB ALBAGHDADI katika Vitabu vyao walieleza kuwa; kipindi ambacho Omar(RA) alimtaka Ally (as)kumuoza Binti yake, ally(AS) alimtuma Ummu Kulthum Kitambaa Msikitini ili Omar(RA) kama atavutiwa na Binti yule, alipoingia na Kitambaa kile Omar(RA) alimpandisha nguo yake hadi kuonekana muundi wake. IBN ATHIR asema: Baada ya Omar(RA) kumpandisha nguo alimshika kwenye paja lake(Ummu Kulthum). DAULABI nae alisema: Baada ya kumpandisha nguo hiyo alimkumbatia(Ummu Kulthum). Ila Sheikh ALHAKIM NAISHABURI NA BAIHAQI hawakupokea maneno kama hayo. Na IBN JAUZI asema: SI VYEMA KUNASIBISHWA MANENO HAYO KWA OMAR(RA), KWA KUWA WAMEKUBALIANA WAISLAMU WOTE KUWA HAIRUHUSIWI KUMSHIKA MWANAMKE AMBAYE WAWEZAKUMUOWA NDANI YA MSIKITINI.
4- Kama kweli ndoa baina ya Ummu Kulthum na Omar(RA) walikuwa na watoto wangapi?!!... baadhi ya riwaya zaeleza kuwa walipata mtoto mmoja aitwa ZAID...Riwaya zengine watoto wawili RUQAIYA na ZAID...SHEIKH NAWAWI katika Kitabu chake cha TAHDHIBUL ASMAA WA LUGHAT alikuwa na watoto wa wili Fatima na Zaid...watoto hao kuna tofauti hadi hii leo.
5- Hata katika kifo chake kuna tofauti na siku ya kuzikwa na aliemsalia ni nani!! Baadhi yao wasema alisaliwa na SAAD IBN ABII WAQAS au HASAN NA HUSEIN au ABDALLAH IBN OMAR au SAID IBN AL-AAS. Ajabu mtoto gani asiye fahamika na Baba yake ni mmoja katika Maswahaba wa kubwa na maarufu wa Mtume(S.A.W.W)!!! Hata siku ya kufariki na aliyemsalia hafahamiki!!.
6- Kwanini izungumzwe siku ya kuowa Omar(RA) ila siku ya kufariki haifahamiki?!, yote ni kutokana na kuwa habari ya kuolewa Ummu Kulthum inautata ndani yake.
intaendelea inshaallah