4 Novemba 2014 - 19:02
Watu 28 wauawa katika maadhimisho ya Ashuraa Nigeria

Watu wanaosadikiwa kuwa ni magaidi wamevamia mashia waliokuwa kwenye maadhimisho ya Imam Husein a.s huku Nigeria na kuua watu ishirini na nane.

Watu wanaosadikiwa kuwa ni magaidi wamevamia mashia waliokuwa kwenye maadhimisho ya Imam Husein a.s huku Nigeria na kuua watu ishirini na nane.
Makatili hao wa walivamia msafara wa maombolezo ya imam husein na kuwamininia risasi waadhimishaji hao na kusababisha vifo vya watu ishirini na nane na wengine themanini kujeruhiwa vibaya.
Mpaka hivi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na mashambulizi hayo ya kikatili, hivyo imebaki gumzo wengine wanadai kuwa ni vikosi vya serikali ndio vilovamia na kumimina risasi na wengine wanasema kuwa ni magaidi wa Boko haram.
Nigeria inahesabika kuwa ni nchi ya kwanza kwa Afrika kwa kuwa na wafuasi wengi wa madhehebu ya shia, na kumeripotiwa kukua kwa kasi dhehebu hili tukufu katika nchi hiyo.
Ikumbukwe kuwa katika ijumaa ya mwisho wa mwezi mtukufu wa ramadhani vikosi vya serikali ya Nigeria vilivamia maadhimisho ya siku ya Qudsi na kuua watu kadhaa wakiwemo watoto watatu wa kiongozi wa mashia wa Nigeria, Sheikh Zakzaki

Tags