Ripoti kutoka vyombo vya habari nchini Israel zinaarifu kuwa wanamgambo wa kundi la Hamas la Palestina walikuwa wamepanga njama ya kumuua waziri wa mambo ya nje wa Israel, Ivgador Lieberman, na walikuwa tayari wamekusanya taarifa kuhusu mienendo yake ili kutekeleza njama hiyo. Mtandao ujulikanao Ynet unaohusishwa na gazeti maarufu la Israel, Yediot Ahronot, umezinukuu duru za jeshi la Israel zikisema kuwa tawi dogo la kundi la Hamas lenye makao yake mjini Bethlehem lilipanga kumuua Lieberman kwa kutumia guruneti la kurushwa kama roketi na lilikuwa limenunua silaha ya kulirushia kombora hilo. Shambulizi hilo lilipaswa kutoa ujumbe kwa Israel kusitisha mashambulizi yake dhidi ya Ukanda wa Gaza yaliyofanyika mwezi Julai mwaka huu ambapo kiasi cha Wapalestina 2,100 waliuawa. Liebereman ndiye afisa pekee wa ngazi za juu serikalini anayeishi katika Ukingo wa Magharibi. Uhasama kati ya Israel na Palestina umezidi katika kipindi cha hivi karibuni baada ya matukio ya waisrael kuchoma masjid ya wapalestina na waparestina kuvamia sinagogi la wa Israel na kuuwa watu wane.
21 Novemba 2014 - 11:36
News ID: 652820
_546f22759bfbb.jpg)
Ripoti kutoka vyombo vya habari nchini Israel zinaarifu kuwa wanamgambo wa kundi la Hamas la Palestina walikuwa wamepanga njama ya kumuua waziri wa mambo ya nje wa Israel, Ivgador Lieberman